Kama Simba mkimsajili George Mpole ndipo nitakapoona jinsi msivyo serious

Kama Simba mkimsajili George Mpole ndipo nitakapoona jinsi msivyo serious

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Huyu ni mchezaji wa kiwango cha kawaida sana.

Haijalishi anaongoza kwa kufunga magoli, ila attitude yake ni changamoto.

Nakumbuka siku moja kuna mchezaji wa Simba kama vile Kanoute alifanya faulo,jinsi Mpole alivyomfuata kumsukuma alifanya kwa hasira kama mtu aliyekuwa amempania siku nyingi.

Pia ilikuwa ni kwa hisia kali kama vile kuna chuki baina yao.

Mimi nilijiuliza swali shida ni nini!? Mbona mtu kama Mayele ni amani sana.

Huyo George Mpole sio size ya Simba labda kama mnamipango ya kushindana na Azam FC
 
uto tulieni dawa iwaingie.

simba inajipanga kimataifa 2022~2023
 
Mpole akikubali kwenda kwenye moja ya hizi timu za Kariakoo itakuwa katanguliza tamaa ya kipato kuliko kuangalia hatma yake binafsi.

Mpole kwa sasa angebaki alipo au aende Timu kama Namungo, Azam au Singida ambapo atacheza akiwa stress free na huku akipata uzoefu zaidi na kuonesha alichonacho ikiwezekana hata baadae akacheze nje ya nchi.
 
Mpole akikubali wkenda kwenye moja ya hizi timu za Kariakoo itakuwa katanguliza tamaa ya kipato kuliko kuangalia hatma yake binafsi.

Mpole kwa sasa angebaki alipo au kwend Timu kama Namungo, Azam au Singida ambapo atacheza akiwa stress free na huku akipata uzoefu zaidi na kuonesh alichonacho ikiwezekana hata baadae akacheze nje ya nchi.
Mpole atakua sawa kwasababu anatafta pesa, lakini watakaopata hasara ni Simba kwa kusajili mchezaji ambaye hatakua na faida kwao.
 
Back
Top Bottom