Kama Taifa ni lazima tujiulize tunatengeneza kizazi cha aina gani? Uchawa unaimaliza nchi

Mtu Alie Nyikani

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2022
Posts
949
Reaction score
2,038
Wakuu habari zenu?

Wakuu nimekaa nimetafakari kuhusu hili jambo linalo itwa "UCHAWA" linavyo shika Kasi ndani ya nchi hii, naliona linaenda kuangamiza Taifa , hasa kwa vizazi vijavyo.

Kwa muda mrefu, mwelekeo wa elimu, malezi, na uongozi umeonyesha mabadiliko makubwa.

Badala ya kujenga kizazi chenye fikra huru, maadili imara, na uwezo wa kushirikiana kujenga taifa, ajabu zaidi kuna ongezeko la vijana wanaotanguliza maslahi binafsi na kuwa tayari kufanya chochote kwa lengo la kufanikisha ajenda zao binafsi.

Jambo ambalo ni hatari kwa Taifa hili hasa kwa vizazi Vyetu.
 
Attachments

  • Screenshot_20250127-162353.jpg
    Screenshot_20250127-162353.jpg
    367.5 KB · Views: 1
  • 20250128_165731.jpg
    20250128_165731.jpg
    310.7 KB · Views: 3
  • Screenshot_20250127-162809.jpg
    Screenshot_20250127-162809.jpg
    380.7 KB · Views: 3
  • Screenshot_20250127-162604.jpg
    Screenshot_20250127-162604.jpg
    244.4 KB · Views: 1
  • Screenshot_20250127-162106.jpg
    Screenshot_20250127-162106.jpg
    433 KB · Views: 1
  • Screenshot_20250127-161900.jpg
    Screenshot_20250127-161900.jpg
    523.1 KB · Views: 3
  • Screenshot_20250127-161807.jpg
    Screenshot_20250127-161807.jpg
    315.2 KB · Views: 1
CCM wako tayari kufanya chochote kile as far as watapata kura....nimeangalia juzi matokeo ya Shule ya sekondari Kiwalani iliyoko Jijini Dar es salaam, ina ZERO 240 Nikaumia sana na kuogopa sana sana. Tunajenga Taifa la ajabu sana
 
Uchawa wa kisiasa ndio hautakiwi,

Ila huu mwingine ni ubunifu unatakiwa na kizazi hiki kutumia vizuri fulsa iliyopo mtandaoni, hususani katika biashara na sanaa.
 
MWALIMU NYERERE ANAMALIZA KWA USHAIRI KWENYE KITABU CHAKE.

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.

Ole wake Tanzania Tusipoisaidia
Niwezalo nimelifanya kushauri na kuonya nimeonya.

tahadhali nimetoa ushauri na kuonya nimeshatoka kitini zaidi nifanye nini.

Namlilia Jaalia atumulikie njia Tanzania ailinde WAOVU wasiishinde.

Amina Tena Amina Amina Tena amina

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.
MWALIMU JK NYERERE
 
Wakuu habari zenu?

Wakuu nimekaa nimetafakari kuhusu hili jambo linalo itwa "UCHAWA" linavyo shika Kasi ndani ya nchi hii, naliona linaenda kuangamiza Taifa , hasa kwa vizazi vijavyo.

Kwa muda mrefu, mwelekeo wa elimu, malezi, na uongozi umeonyesha mabadiliko makubwa.
Badala ya kujenga kizazi chenye fikra huru, maadili imara, na uwezo wa kushirikiana kujenga taifa, ajabu zaidi kuna ongezeko la vijana wanaotanguliza maslahi binafsi na kuwa tayari kufanya chochote kwa lengo la kufanikisha ajenda zao binafsi.

Jambo ambalo ni hatari kwa Taifa hili hasa kwa vizazi Vyetu.
Tunahitaji viongozi wenye uwezo wa kutambua na kukemea vikali uchawa. Viongozi wetu wengi wanapenda kuabudiwa na kusifiwa kwa kila wanachofanya, hata kama wamekosea! Matokeo yake hujikuta wamezungukwa na machawa badala ya watu wenye uwezo na weledi wa kazi walizowapa au wanazowapa.
 
Kodi za wananchi zinatapanywa kwa mgongo wa kumpongeza mtu siku yake ya kuzaliwa!

Hivi angefanya kusherekea faragha na mumewe angepungukiwa nini ?

Maana kikatiba hakuna maadhimisho ya hivi ila hao machawa wako busy kutumia kodi na huyo rais akipotea siku kadhaa watu wakianza kuhoji yuko wapi au ni mzima kiafya vitisho vinaanza wakati hili sasa lipo kikatiba .
 
Wakuu habari zenu?

Wakuu nimekaa nimetafakari kuhusu hili jambo linalo itwa "UCHAWA" linavyo shika Kasi ndani ya nchi hii, naliona linaenda kuangamiza Taifa , hasa kwa vizazi vijavyo.

Kwa muda mrefu, mwelekeo wa elimu, malezi, na uongozi umeonyesha mabadiliko makubwa.

Badala ya kujenga kizazi chenye fikra huru, maadili imara, na uwezo wa kushirikiana kujenga taifa, ajabu zaidi
Ndugu uangu zamani hizo tulikuwa na mabaraza ya vijana ambayo yalitambulika kama MATANURU YA FIJRA, sasa hivi tunajenga MATANURU YA CHAWA!
 
Ili nalo mkalingalie.....
Tunaomba uchawa iwe kozi inayofundishwa katik vyuo nchini.
 
CCM wanapenda story hz.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Kodi za wananchi zinatapanywa kwa mgongo wa kumpongeza mtu siku yake ya kuzaliwa!

Hivi angefanya kusherekea faragha na mumewe angepungukiwa nini ?

Maana kikatiba hakuna maadhimisho ya hivi ila hao machawa wako busy kutumia kodi na huyo rais akipotea siku kadhaa watu wakianza kuhoji yuko wapi au ni mzima kiafya vitisho vinaanza wakati hili sasa lipo kikatiba .
Hapo kwenye "na mumewe" baaaas umetisha, iwe hvyo tu
 
Wakuu habari zenu?

Wakuu nimekaa nimetafakari kuhusu hili jambo linalo itwa "UCHAWA" linavyo shika Kasi ndani ya nchi hii, naliona linaenda kuangamiza Taifa , hasa kwa vizazi vijavyo.

Kwa muda mrefu, mwelekeo wa elimu, malezi, na uongozi umeonyesha mabadiliko makubwa.

Badala ya kujenga kizazi chenye fikra huru, maadili imara, na uwezo wa kushirikiana kujenga taifa, ajabu zaidi kuna ongezeko la vijana wanaotanguliza maslahi binafsi na kuwa tayari kufanya chochote kwa lengo la kufanikisha ajenda zao binafsi.

Jambo ambalo ni hatari kwa Taifa hili hasa kwa vizazi Vyetu.
Nakazia. Uchawa sasa ni adui wa nne wa Taifa letu, baada ya ujinga, umaskini na maradhi!
 
Wakuu habari zenu?

Wakuu nimekaa nimetafakari kuhusu hili jambo linalo itwa "UCHAWA" linavyo shika Kasi ndani ya nchi hii, naliona linaenda kuangamiza Taifa , hasa kwa vizazi vijavyo.

Kwa muda mrefu, mwelekeo wa elimu, malezi, na uongozi umeonyesha mabadiliko makubwa.

Badala ya kujenga kizazi chenye fikra huru, maadili imara, na uwezo wa kushirikiana kujenga taifa, ajabu zaidi kuna ongezeko la vijana wanaotanguliza maslahi binafsi na kuwa tayari kufanya chochote kwa lengo la kufanikisha ajenda zao binafsi.

Jambo ambalo ni hatari kwa Taifa hili hasa kwa vizazi Vyetu.
Tunao waamini ndio wanasema hii njia ndio iliyo sahihi, kama walivyopitisha majina tarajiwa kwa uchafuzi wa oktoba
 
Inaumiza sana sanaaa, kila mtu sasa ana picha ,ana kofia , nahisi mpaka chupi wanazo,

Sio mbaya kuwasifu wanasiasa ila hii sasa ni too much tooo much katika umri wangu huu sijawahi kuona uchawa ukitamalaki kama miaka hii

Ashakum si matusi tunaenda pabaya sana sanaaa tusipoangalia.
 
Hao machawa watakabiliana na hiki 👇

"Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kinga yake huku moyoni mwake amemwacha Mungu" Yeremia 17:5
 
Back
Top Bottom