Kuna suala la hawa Wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA ambalo wote naona tunalisahahu kulidadavua.
Ibara ya 78(4) ya katiba ya Tanzania inasema hivi
"Orodha ya majina ya wagombea wanawake iliyowasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi na kila chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu ndiyo itakayotumiwa na Tume ya Uchaguzi baada ya kushauriana na chama kinachohusika, kwa madhumuni ya kujaza nafasi yoyote ya Mbunge wa aina hii inapotokea wakati wowote katika maisha ya Bunge."
Hapa kuna matukio mawili.
Kwanza kuna tukio la Tume kushauriana na chama, hivyo Tume inatakiwa kuwa ilishauriana na CHADEMA. Pili kuna tukio la kupokea majina ya Wabunge hao kutoka kwenye chama. Hapa ndipo tumesikia utetezi wa Tume kwamba walipokea majina kutoka CHADEMA tarehe 19 Novemba 2020.
CHADEMA waeshautangazia ulimwengu kwamba hawajafanya lolote kuhusu Viti Maalum. Hebu tu assume tumewapuuza CHADEMA na tukaamini labda Mnyika alipeleka hayo majina hiyo terehe 19 Novemba. Bado Tume hata tukiamini hivyo hawasemi tukio la kushauriana na CHADEMA walilifanya lini.
Huku CHADEMA wanasema hawajawahi kufanya mchakato wowote wa majina ya Viti Maalum. Tume wanasema mchakato umefanyika kisheria, yaani walipokea majina tarehe 19. Narudia wanasema tukio la kupokea tu majina, mimi lile tukio la kushauriana silioni popote katika taarifa ya Tume.
Maana tukio la kushauriana linaambatana na matokeo ya kushauriana.
Mnalionaje hili