Inasikitisha kuona shirika la habari la Taifa (TBC) linashindwa kuonesha mechi muhimu ya Timu yetu ya Taifa. Na kutegemea shirika binafsi kuonesha.Duniani kote Shirika la umma ndilo linapaswa kuwa la kwanza kutumia njia yoyote ile ili kuonesha tukio la kitaifa.Hivi TBC na TFF mnafikiria nini katika hili? ni lazima mjue Taifa Stars ni timu ya watanzania wote na si wakazi wa Dar es Salaam tu.Mnapaswa kuhakikisha mnafikia makubaliano na kuwapa raha watanzania.Leo mmenisikitisha sana kutokuonesha mechi hii muhimu.Hivi mnafikiri ni kwa nini watu wanapenda sana ligi ya ulaya..hasa uingereza...moja ya sababu (pamoja na kuwa ni bora) ni kutangazwa sana. Sasa nyie mnafikiri sisi wa vijijini tutaipenda vipi Taifa Stars bila ya kuiona ikicheza???