Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Waulize akina Chifu Songea Mbano na Mababu zetu wengine walionyongwa kwenye mibuyu.Wakoloni hawakuwa fungal au kuwanyonga kina Nyerere au Mandela.
Wakoloni wasingepita na Mdude, Soka, Polepole au hata kumtendea Lissu hivi.
Waulize akina Chifu Songea Mbano na Mababu zetu wengine walionyongwa kwenye mibuyu.
Lengo langu ni kueleza kuwa Wakoloni waliua sana, Wajerumani wameacha makaburi ya halaiki kote Tanganyika kwahiyo kusema wakoloni weupe walikuwa wazuri ni upotoshaji.Nimekuuli za kina Nyerere, Mandela, na wa namna hiyo kwa makusudi mazima kuwa wakipigania haki zao waziwazi kwa amani kama Lissu, Polepole, Soka, Mdude na wengi wao. Majibu yako tafadhali.
Lengo langu ni kueleza kuwa Wakoloni waliua sana, Wajerumani wameacha makaburi ya halaiki kote Tanganyika kwahiyo kusema wakoloni weupe walikuwa wazuri ni upotoshaji.
Sema na hivi vyama vya uhuru navyo vimeanza kuiga mbinu za wakoloni baada ya kuona vimechokwa
Hakuna unafuu wowote mfano wa Mandela kuachiwa ni pressure kutoka katika mafaifa ya nje.Lengo langu ni kueleza hawakuwa wema lakini walikuwa na nafuu.
Hawakuwauwa au kuwafunga wapigania haki kwa amani.
Kama siku zile kama leo waungwana waliuzwa na wenzao kama walivyokuwa wakifanya waliokwenda shaumma au wanavyoendelea kufanya masalio yao leo.
Ogopa sana wasaliti na hasa wa ndani!
Hakuna unafuu wowote mfano wa Mandela kuachiwa ni pressure kutoka katika mafaifa ya nje.
Lakini waliua sana Steve Bantu Biko,Chris Hani na wengine wengi sana.
Hata Kiswahili hujui, mtanzania wewe au mkimbizi tuu…yako sio wakoWrite your reply...ndumku wa mama kowa
Kweli kabisa, aniulize Mimi nimwambie mambo yalivyokuwa.Waulize akina Chifu Songea Mbano na Mababu zetu wengine walionyongwa kwenye mibuyu.
Mara nyingi katika mijadala ya kisiasa nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla, lawama nyingi hupelekwa kwa vyama tawala kama vile CCM, kana kwamba matatizo yote ya kijamii na kiuchumi yanatokana na uongozi wao. Hata hivyo, hoja ya msingi inabaki kuwa si chama pekee kinachoshikilia mizizi ya matatizo ya bara letu, bali mfumo wa dunia uliojengwa katika msingi wa ukoloni wa kiuchumi unaoendelea hadi leo.Eti Amani !! amani, amani!!! Hii Tanzania kuna amani au kisiwa cha uvumilivu??? CCM ilipo sasa, kwa udhalimu wake, imetutoa kwenye kisiwa cha amani imetupeleka kwenye kisiwa cha uvumilivu. Je sisi vijana tupo tayari vizazi vyetu vije viishi kwenye kisiwa cha uvumilivu kama sisi??
Tukumbuke wazee wetu walivyojitoa bila kujali silaha za Muingereza, ili tu sisi tupate uhuru. Kwa nini sisi tunashindwa kupambania kizazi chetu kijacho, kisiishi maisha ya kidhalimu yanayoendeshwa na serikali ya CCM ???
CCM inasema vita vita, wao mbona waliandamana kwa Muingereza na vita haikutokea. Muingereza na bunduki zake na mizinga lakini wao waliendelea kuandamana bila kuogopa vitisho vya vifo, mpaka Muingereza akawapatia kile wanachotaka??? Yaani watu wanatekwa, damu zinamwagika, bado tu wananchi tunanyamaza??? Ni kitu gani duniani kina thamani kuliko uhai wa watu ??
Serikali inadidimiza uchumi, inauza rasilimali za taifa kiholela huku anazidi kuongeza deni la taifa ambalo litaathiri mpaka vizazi vijavyo. Tunamuangalia tu ??? Sisi ni wabinafsi kiasi gani mpaka tunashindwa hata kujitoa kwa ajili ya vizazi vyetu?? 29 OKTOBA tudai hatma ya taifa letu. KATIBA MPYA ni sasa. Mwisho wa UFISADI ni sasa. Mwisho wa UTEKAJI na UUAJI ni sasa.
Wewe ndio akili yako bado imelala kwa Wakoloni. Kuwaondoa Wamasai kwenye ardhi yao ni Mkoloni?? Kuuza bandari kwa muwekezaji uchwara ni Mkoloni?? Kuwabambikia kesi ndugu zako tena wa damu ili tu uwadhoofishe kisiasa ni Mkoloni?? Kuwateja na kuwapoteza raia wa nchi yako mwenyewe ni Mkoloni?? Kujilimbikizia ukwasi wa kutisha kwa fedha za umma kisa madaraka uliyonayo nayo ni Mkoloni??Mara nyingi katika mijadala ya kisiasa nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla, lawama nyingi hupelekwa kwa vyama tawala kama vile CCM, kana kwamba matatizo yote ya kijamii na kiuchumi yanatokana na uongozi wao. Hata hivyo, hoja ya msingi inabaki kuwa si chama pekee kinachoshikilia mizizi ya matatizo ya bara letu, bali mfumo wa dunia uliojengwa katika msingi wa ukoloni wa kiuchumi unaoendelea hadi leo.
Baada ya uhuru wa kisiasa katika miaka ya 1960, mataifa ya Afrika yalipata kile kinachoitwa uhuru wa bendera — uwezo wa kuinua bendera na kuwa na wimbo wa taifa — lakini hayakupata uhuru wa kiuchumi. Mifumo ya kifedha, kisheria, kielimu na kibiashara ilibaki ikidhibitiwa na taasisi na mataifa yaliyokuwa makoloni. Matokeo yake, tunajikuta bado tukiishi katika “nyumba ya kupanga” — ardhi yetu, rasilimali zetu, na nguvu kazi yetu, lakini hatuna mamlaka kamili ya kuamua namna ya kuzitumia kwa faida ya watu wetu.
Leo hii, Afrika inauza malighafi kwa bei ndogo na kununua bidhaa zilizokamilika kwa gharama kubwa. Bei ya dhahabu, mafuta, pamba, au kahawa inaamuliwa katika masoko ya nje, si katika nchi zinazozalisha. Hata mikopo na misaada inayotolewa kwa mataifa yetu mara nyingi huambatana na masharti yanayolazimisha utekelezaji wa sera zinazolinda maslahi ya watoa mikopo badala ya wananchi wa Afrika.
Wale viongozi wachache waliothubutu kupinga mfumo huu — kama Thomas Sankara, Patrice Lumumba, na Muammar Gaddafi — waliondolewa madarakani au kuuawa kwa mikono ya nguvu za kimataifa. Hii inaonyesha kuwa tatizo la Afrika si uongozi wa mtu mmoja au chama fulani, bali ni mfumo wa utegemezi uliopangwa makusudi kutuacha tukiwa watumwa wa kiuchumi katika ardhi yetu wenyewe.
Suluhisho haliko katika kubadilisha vyama tu, bali katika mabadiliko ya kifikra na kiuchumi: kuwekeza katika uzalishaji wa ndani, elimu bunifu, teknolojia, na umoja wa bara la Afrika katika maamuzi ya uchumi. Ni hapo tu ndipo tutakapoweza kusema tumevuka kutoka katika uhuru wa bendera kwenda kwenye uhuru wa kweli wa kiuchumi na kifikra.