Mkaa wa mawe
JF-Expert Member
- Jun 28, 2020
- 5,055
- 7,496
Kila mtu na fikra zake, una uhuru wa kuwa na fikra hizo ulizokuwa nazo. Nami nina mtazamo wangu wa haya matatizo tuliyokuwa nayo, na nina imani hakuna chama wala kiongozi atakayeweza kutatua haya matatizo yetu si kwa Tanzania pekee bali Afrika nzima. Na njia nzuri ni mabadiliko ya kifikra na kiuchumi, kuwekeza katika uzalishaji wa ndani, elimu bunifu, teknolojia, na umoja wa bara la Afrika katika maamuzi ya uchumi.Wewe ndio akili yako bado imelala kwa Wakoloni. Kuwaondoa Wamasai kwenye ardhi yao ni Mkoloni?? Kuuza bandari kwa muwekezaji uchwara ni Mkoloni?? Kuwabambikia kesi ndugu zako tena wa damu ili tu uwadhoofishe kisiasa ni Mkoloni?? Kuwateja na kuwapoteza raia wa nchi yako mwenyewe ni Mkoloni?? Kujilimbikizia ukwasi wa kutisha kwa fedha za umma kisa madaraka uliyonayo nayo ni Mkoloni??
Hayo yote uliyoyazungumza hayana tija bali ni fikra mgando. Huna tofauti na mtu aliyeambiwa daraja ni bovu asipitishe gari. Yeye akashupaza shingo. Kafika katkati daraja limekwenda pamoja na yeye. Kanusurika kifo, anaulizwa kulikoni eti anamsingizia shetani. Upuuzi mtupu.
Hakuna unafuu wowote mfano wa Mandela kuachiwa ni pressure kutoka katika mafaifa ya nje.
Lakini waliua sana Steve Bantu Biko,Chris Hani na wengine wengi sana.
Wakoloni wa kiarabu walichukua maelfu ya Watumwa wakoloni wa Kijerumani walikuwa wakinyonga mababu zetu kwenye mibuyu
Wakoloni wa kiarabu walichukua maelfu ya Watumwa wakoloni wa Kijerumani walikuwa wakinyonga mababu zetu kwenye mibuyu