Kama tumekubaliana kwamba wanaopata ujauzito waendelee basi na baba mtoto asamehewe walee mtoto

Kama tumekubaliana kwamba wanaopata ujauzito waendelee basi na baba mtoto asamehewe walee mtoto

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau!

Hili ni jambo jema sana pongezi kwa mheshimiwa rais Samia Hassan.

Ila nilikuwa namuomba rais kupitia kiti chake aliombe bunge kuangalia upya ile sheria ya kale kamshikaji kalichopelekea mwanafunzi kupata ujauzito basi wasiwe wanafungwa jera wanaweza pewa tu adhabu ya faini.

Hii itasaidia katika kujenga saikolojia ya mama na pia mtoto kupata malezi bora. Kwa ss tulioishi nje ya nchi tunafahamu kwamba nchi zingine hakuna kifungo kama ukimpa mwanafunzi ujauzito maana ni jambo la kheri.

ila unapomfunga mzazi mmoja unakuwa unampokonya haki ya mtoto kupata malezi ya wazazi wote wawili pia kisaikolojia na kiuchumi mama anaathirika maana baba anakuwa ndio mlezi just imagine mtu ana mtoto harafu yupo peke yake analea mtoto.

Mwisho jera zetu zinajaa bure tu ,kwani moja ya maagizo ya Mungu kwa mwanadamu ni kuzaa na kuijaza dunia sisi ni nani wa kupingana na maagizo ya Mungu.

#Tuwaache huru wasome na waijaze dunia.
 
That means unahalalisha wanafunzi kulalana shuleni
Try to be serious my friend
Acha mfumo jike utawale mfumo dume umechemka sana kwa takribani miaka 6
 
That means unahalalisha wanafunzi kulalana shuleni
Try to be serious my friend
Acha mfumo jike utawale mfumo dume umechemka sana kwa takribani miaka 6
Kuna sheria mbili hapa boss ,kuna ile ya mtu anayeshiriki na binti wa chini ya 18 (mtoto) na kuna sheria ya kumpa mimba mwanafunzi namaanisha iliwa mwanafunzi ni above 18 huyo ni mtu mzima hivyo atakuwa amefanya maamuzi sahihi .
 
That means unahalalisha wanafunzi kulalana shuleni
kulalana mbona wanalalana saana tu, tunachotakiwa kuwafundisha hawa teen's sisi kama wazazi na walezi ni namna ya kwamba wasipeane mimba, kulalana huwezi kuzuia kwani hilo ni fumbo la imani - mtu akishabarehe tu suala hilo ni vigumu kulizuia bali jikite kutoa mafunzo ya elimu ya uzazi kwisha.
 
Sex with a minor ni sawa na rape tu sababu umetake advantage ya udogo wake kumuingilia hiyo itabaki hivyo.

Sasa binti aliyedanganywa na kubakwa kwa definition hiyo ya hapo juu anastahili adhabu ya kunyimwa haki ya kusoma??

Siungi mkono mimba za udogoni lakini adhabu iwe fine au kunyimwa ajira serikalini etc lakini sio kukosa elimu.

Ssa ana mtoto na hana elimu ataendeshaje maisha bila kuwa na reasoning inayokuja na maarifa ya shuleni??

Adhabu hata siku moja haipaswi kupingana na haki ya elimu kwa mhusika ambaye pia ni muhanga wa ''kubakwa''.
 
kulalana mbona wanalalana saana tu, tunachotakiwa kuwafundisha hawa teen's sisi kama wazazi na walezi ni namna ya kwamba wasipeane mimba, kulalana huwezi kuzuia kwani hilo ni fumbo la imani - mtu akishabarehe tu suala hilo ni vigumu kulizuia bali jikite kutoa mafunzo ya elimu ya uzazi kwisha.
Umeongea point boss,genye ni kibiolojia unaweza sema involuntary action😂😂😂yaani kama kupiga chafya vile zikikupanda ngumu kujizuia kama haujafundishwa jinsi ya kuzi control
 
Basi ile Sheria ya miaka 30 jela kwa watia mimba iondolewe tu nayo maana haitokua na maana hata.
kwani mtu mzima akibaka huwa anaachiwa kisa tu aliyempa mimba ni mtu mzima??

Jinai ni jinai tu na haki ya muhanga wa mimba pia zilindwe. Kwani lazima adhabu iwe kufukuzwa shule? Kwanini mnalazimisha binti anyimwe elimu. Kwanini hamuongelei walau fine kubwa?
 
Kwa akili zako unafikiri vibinti vya shule siku hizi vinapata mimba kwa kubakwa??
 
That means unahalalisha wanafunzi kulalana shuleni
Try to be serious my friend
Acha mfumo jike utawale mfumo dume umechemka sana kwa takribani miaka 6
Hapana hapa ina maanisha adhabu itafutwe mbadala na sio kumnyima elimu mtoto wa kike ambaye mpaka ssa yupo nyuma kielimu kuliko mwanaume.

Msifungamanishe kosa la mimba na adhabu ya kunyimwa elimu havina correlation kabisa. Ni sawa na viboko huwa watu wanakasirika wakisikia vinaondolewa yaani kana kwamba hakunaga adhabu mbadala hivi!! Tusikariri wakuu wanaweza kuja na adhabu tofauti ambayo itakua funzo ila wakati huo huo haimnyimi fursa ya elimu mtoto wa kike.
 
Kwa akili zako unafikiri vibinti vya shule siku hizi vinapata mimba kwa kubakwa??
Nimesema taking advantage? Binti wa form two ukimnunulia chips mara 3 tu inatosha kumwambia aje room kwako anakubali!!

Hyo taking advantage ndio tunaigeuza Rape. Ndio maana ukimwambia I love u anapagawa tofauti na binti wa miaka 25 ambaye keshaambiwa a millio times na wanaume.
 
Hiyo ni 'Fair and square" mkuu....kifungo cha miaka 30 jela ni uonevu mkubwa ikiwa binti atarudi kuendelea na shule. Labda ithibitike kuwa kweli alipewa ujauzito kwa kubakwa.
Kwanini uonevu? Sex with a minor ni rape

Whatever adhabu ya alipewa mimba itakavyokua haina correlation na kosa la mbakaji kumlala mtoto!!

Kwanini mnafungamanisha?
 
afande selle hili haliwezekani, lazima wanaofanya huu uharibifu wakione cha moto.
Lkn inaonekana kama wewe ni sehemu ya uharibifu huu afande selle.
 
waowane kwa lazima tuu bila kuachana ndani ya miaka 10 ,wakiachana chini ya hapo dume afungwe jela miaka 30.
Lalbda Msichana akaombe talaka Mahakamani na akubaliwe na Mahakanma tu endapo sababu zake zitakuwa za msingi.
 
Sex with a minor ni sawa na rape tu sababu umetake advantage ya udogo wake kumuingilia hiyo itabaki hivyo.
Mkuu, hao minor wanaowatega/wanaochochea ngono kwa seniors wa kiume wao sheria inawaangalia vp?

Men are visual being ndio maana uarabuni mwanamke anafunika mwili wake mzima.
 
kwani mtu mzima akibaka huwa anaachiwa kisa tu aliyempa mimba ni mtu mzima??

Jinai ni jinai tu na haki ya muhanga wa mimba pia zilindwe. Kwani lazima adhabu iwe kufukuzwa shule? Kwanini mnalazimisha binti anyimwe elimu. Kwanini hamuongelei walau fine kubwa?
Adhabu inapaswa kuwa kwa wote walioshiriki tendo la ngono.
 
Back
Top Bottom