Kama tunahitaji kupata fedha nyingi kwanza ni lazima tuboresha aina ya huduma tunazotoa

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
“ILI KUPATA FEDHA LAZIMA UWE NA KITU CHA KUUZA.”

Bila kumung’unya maneno, nafikiri wote tutakubaliana na tafsiri ya fedha kama njia ya kubadilishana bidhaa au huduma baina ya mtu mmoja na mwingine au jamii moja na nyingine n.k. Kwa lugha nyepesi ili kupata fedha lazima uuze kitu kwa mtu mwingine. Hiki kitu kinaweza kuwa ni nguvu zako, akili, muda, bidhaa, huduma, taarifa, maneno, vichekesho, wengine uuza miili yao na vitu vingi vinavyofanana na hivyo.

Kama utakubaliana na mimi kwamba ili kupata lazima uuze kitu, Swali muhimu ambalo unatakiwa kujiuliza kila unapoamuka “je hivi mimi hapa nilipo nauza nini?, Hii ofisi ninayoifanyia kazi nauza nini hasa?,Je hii fedha nimepokea baada ya kuuza kitu gani?,Je haya malipo yanalingana na bidhaa au huduma ninayotoa? Je hiki ninachokiuza naweza kukiboresha ili kilipe zaidi?.

Kama umeajiriwa tambua kuna kitu mwajiri ananunua kutoka kwako, hivyo tafadhali usiseme wewe sio mfanyabiashara. Ndio maana wewe huko hapo kwenye hiyo ajira lakini wazazi wako wapo sehemu nyingine. Hata mimi sipo hapo ulipo wewe, kwa sababu sina uwezo wa kuuza bidhaa kama yako. Na kwa taarifa yako, wanakulipa kila siku sema tu wanakukusanyia na kukupa mwisho wa mwezi. Sio kwamba wanakupenda sana, bali wananua bidhaa au huduma kutoka kwako.

Kama unalipwa fedha kidogo, hakuna haja ya kulalamika bali tambua ya kwamba bidhaa unayouza haina thamani. Na haina thamani kwa sababu watu wanaouza bidhaa kama yako wapo wengi mtaani, hivyo ukikataa kumuuzia kesho atakwenda sokoni ananunua nyingine inayofanya kazi tena zaidi ya kwako kwa gharama nafuu kabisa. Ukiona unalipwa kiasi kikubwa zaidi, tambua bidhaa au huduma unayoitoa ina upekee kidogo na haipatikana kiurahisi, yaani ni adimu. Hivi wewe haujawahi kujiuliza kwa nini dhahabu na almasi zinauzwa kwa bei ghali?, Jibu ni kwamba vitu adimu.

Natambua fedha tunazihitaji, lazima tuhakikishe tunaboresha bidhaa tunazouza. Bahati kila mtu hapa duniani ana bidhaa au huduma anayouza. Na usiseme hapo ulipo kuwa hauna kitu cha kuuza. Kama unapokea fedha tambua kuna kitu umeuza ndio maana hiyo fedha imefika kwako. Bidhaa ikiwa bora sokoni watu wako tayari kulipia kwa gharama yeyote ile ili waipate.Ikikoswa ubora watu watalipia kiasi kidogo cha fedha.

Hivyo basi, Kama tunahitaji kupata fedha nyingi kwanza ni lazima tuboresha aina ya huduma tunazouza. Kama umeajiriwa angalia namna ya kuboresha uwezo wako binafsi katika hilo eneo (persona skills) ili uwe bora zaidi. Ukiwa bora watu watajitokeza kununua bidhaa, huduma, akili, ujuzi wako huo nawe unatajipatia fedha zaidi ya awali. Kinachonifurahisa ni kuwa hivi vyote vipo ndani ya uwezo wako.

SIKIA SAUTI ILIYONDANI YAKO

Kwa niaba ya Kamara Gombe
 
Dah! Umezungmza kitu POINT sana, nami naongezea ukitaka kulielewa hili vizuri hebu waangalie wachezaji mpira wale wanalipwa kulingana na thamani zao, kadiri ya "huduma" yako inavyokua kubwa katika timu yako ndivyo thamani yako inavyozidi kupanda! Mo Salah thamani yake inazidi kupanda sababu ya kiwango chake kinavyozidi kupanda Liverpool si ajabu akaja kuuzwa kwa kuvunja rekodi za usajili timu nyingne kubwa duniani zitakapo taka huduma yake!.
 
Safi sana mkuu, kuna kipindi siasa tunaweka pembeni na kuleta thread kama hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…