Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Ni dhahiri bila elimu iliyobora maendeleo na amani ya nchi yetu itakuwa matatani. Ili taifa lolote lile liwe na amani ya kudumu watu wake lazima wawe na elimu.
Elimu ni kitu gani hiki ambacho nasisitiza ni muhimu Sana kwa taifa lolote kuendelea? Na kuendelea ni nini? Wote tunatambua kwamba maendeleo ni vitu, ambavyo vinasaidia maisha ya mtu kuwa yenye urahisi na kuondokana na ugumu wa maisha.
Lakini matokeo ya maendeleo yeyote ni elimu, bila maarifa taifa letu alitoweza kupiga hatua katika maendeleo yake na ni ndoto. Ni elimu pekee yenye uwezo wa kufanya mapinduzi katika taifa letu.
Kwahiyo ni muhimu Sana kuangalia elimu yetu Kama ni bora na kama inatengeneza RAIA waliobora ambao watalitumikia taifa lao bila ubinafsi.
Tabia za watu wetu lazima zijengwe kwasababu pasipo kujenga watu wetu katika tabia zilizo bora ambazo zitasaidia ujenzi wa taifa hili, tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu. Hatutaweza kujenga taifa hili.
Ni muhimu sana elimu yetu kujenga watu wetu katika uzalendo, kuleta watu wetu katika utaifa. Na watu wetu waweze kutumia elimu yao ili kuendeleza taifa letu na watu wake. Elimu yetu ya sasa imejengwa katika misingi ya kibinafsi.
Jamii yeyote iliyoelimika hupimwa katika nidhamu na maadili ya watu wake, kwa hakika kabisa nidhamu huleta dira, iwe kwa mtu binafsi au kwa taifa. Ni muhimu kuzingatia nidhamu hii katika taifa. Nidhamu huleta ORDER.
Misingi hii ya elimu ni muhimu sana, elimu ya uzalishaji pasipo vionjo vingine hivi haitasaidia, ni wakati sasa kuuvua ubinafsi. Watoto wetu wakielimika tutakuwa na uhakika wa amani na kuendelea kuwepo kwa taifa letu. Wataweza kufanya vitu sahihi kwa taifa letu kwahiyo tutakuwa na uhakika na baadae ya taifa letu. Maadili ni jambo la msingi sana. Elimu bila maadili ni sawasawa na mto bila kingo.
Bila nidhamu na maadili hakuna familia itakayosimama na Kama familia zitakuwa hazijasimama itakuwa vigumu Sana kwa serikali kutawala. Maadili katika familia ni msingi wa maadili ya kitaifa. Wakuu wa familia wanasaidia kwa kiwango kikubwa serikali kutawala kama ni wa hovyo nchi itakuwa ya hovyo. Familia ni sehemu ndogo ya utawala katika nchi. Kwahiyo maadili ya familia ni muhimu Sana ili kujenga taifa lenye nguvu.
Kwahiyo elimu yetu lazima ianzie nyumbani kwenye makuzi kwa kulea watoto wetu kwa nidhamu na maadili na itaendelea shuleni kwa kumpa maarifa ya kazi na nidhamu katika kazi.
Bila nidhamu hatuta heshimiana na uongozi utakuwa mgumu Sana, hatutasikilizana na tutashindwa kufikia maendeleo yetu ambayo yanahitaji ushiriki wa kila mtu.
Kwahiyo tuna tatizo hili la nidhamu katila taifa letu ambalo kiongozi yeyote mwenye maono ataliona kirahisi na ni ngumu Sana kwetu kuendelea pasipo kulitibu.
Kwahiyo maombi yangu ni kwa watu wa taifa hili kufikiria upya kuhusu utaifa wao hasa viongozi. Tuache ubinafsi na tufikirie watu kwa njia hiyo pekee taifa letu litaendelea. Akili yenye ubinafsi haiwezi kufikiria maendeleo ya watu hata kidogo. Inajiwazia maendeleo binafsi ni akili yenye choyo na haiwezi kuleta amani na maendeleo katika nchi. Ni akili isikuwa na maono
Popote penye ubinafsi kuna vurugu na fujo hakuna amani hata kidogo. Njia tunayoamua kuifanya mapito yetu kwa sasa ni hatari. Sio njia ya kuleta order katika nchi. Naongea na viongozi sababu wao ndio wenye uwezo wa kuleta mabadiliko kama watabadili nia zao.
Ni muhimu sana kuweka taifa letu mbele sio sifa binafsi, cheo, na hata fedha Kama tunataka kusonga mbele lazima tutumikie.