Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA aliyejirejesha CCM na kupewa ubalozi kabla ya kuenguliwa na Samia Suluhu Hassan, Dk Wilbrod Slaa alisikika akijifanya kukipenda CHADEMA hadi kutaka kushiriki kupiga kampeni kwenye uchaguzi wake. Je ana nini au alisahau nini CHADEMA? Inawezekana mwana CCM kama Slaa kuwa na lolote laheri kwa CHADEMA alichohama baada ya kukisaliti alipoahidiwa cheo? Kama tutakuwa wakweli, Dk Slaa bado anaaminika kama alivyo. kabla ya kutimkia CCM? Je itakuwaje ukisikia mtu kama Peter Msigwa akidai anataka demokrasia ndani ya CHADEMA? Kwanini hawa vyangu wa kisiasa hawashinikizi demokrasia. ndani ya chama chao CCM?