SoC01 Kama tutayapuuza mazingira yetu, tutayaharibu maisha yetu

SoC01 Kama tutayapuuza mazingira yetu, tutayaharibu maisha yetu

Stories of Change - 2021 Competition

DustBin

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2021
Posts
609
Reaction score
604
Watu waliostaarabika kimaadili na mienendo huhifadhi mazingira yao kwa kutambua kuwa kufanya hivyo ndio kuhifadhi maisha yao. maana sahihi ya neno mazingira, ni kila kitu kinachomzunguka mwanadamu pale anapoishi. Mazingira hujumuisha mazingira ya nchi kavu, mazingira ya angani na mazingira ya majini. Hivyo maisha ya mwanadamu hutegemea kwa asilimia zote mazingira aliyomo. Kama mazingira yakiwa mabaya basi na maisha huwa mabaya pia na kinyume chake ni hivyo hivyo.

Nimefikiria kubuni kichwa cha habari hiki ili niweze kuwatanabahisha watu ya kwamba, kama tutakua mstari wa mbele kuyaharibu mazingira yetu na tukayapuuza pasi na kufanya juhudi zozote za kuyahifadhi na kuyatunza basi tujue kwa yakini kabisa kwamba tutakua tunayaharibu maisha yetu na maisha ya viumbe wengine tunaoishi nao katika mazingira hayo. Mwisho wa siku kuifanya dunia sio mahala salama pa kuishi.

Nilipata kusikia kauli moja kutoka kwa wahenga wakisema “masaibu tunayoyapata katika maisha yetu ni matokeo ya machumo ya mikono yetu.” Kauli hii ninaiunga mkono kwa asilimia zote hasa nikiilinganisha na mada yangu hii ya leo.

Ingawa duniani tunaishi viumbe vingi, lakini mwanadamu ndiye aliyepewa utashi na mamlaka ya kuyamiliki mazingira na hata kuvimiliki/kuvidhibiti viumbe vingine. Hivyo basi ni wazi kwamba jukumu la kuhifadhi mazingira yetu ni la mwanadamu mwenyewe aliyepewa uelewa na akili. Badala yake mwanadamu amekua jeuri, asiyejali maisha yake na hata maisha ya viumbe wenzake wanaomtegemea. Badala ya kuyatunza mazingira mwanadamu amekua ndio mchafuzi na mharibifu namba moja. Ili waishi kwa amani na raha Viumbe hawa wanahitaji hewa safi, ardhi safi, maji safi, chakula safi, mwanga wa kutosha, giza lenye manufaa, joto lenye tija, baridi isiyodhuru, nk. Ni jukumuu la mwanadamu kuhakikisha yote hayo yanapatikana ili kuifanya sayari ya dunia kuwa ni mahala pazuri pa kuishi.

Kuongezeka na kukua kwa shuguli za mwanadamu kumechochea kuharibu mazingira yetu. Kutokana na shuguli hizo ardhi ikapoteza rutuba hivyo kusababisha ukosefu wa chakula cha kutosha, hewa ikachafuliwa magonjwa yasiyotibika yakaongezeka viumbe wakapoteza uhai, ardhi ikawa jangwa na kame mvua zikaadimika mimea ikakosa kustawi viumbe kama wanyama wakakosa malisho. Cha ajabu mwanadamu amejisahau moja kwa moja akawa hana mpango wa kuhifadhi mazingira yake. Mfano wa karibu, mchunguze kijana wa kileo, kisha tazama hata sehemu anapolala atakua amepapuuza, hana muda hata wa kutandika kitanda chake ambacho kwacho ndio anapata usingizi mnono akili yake ikatulia. Hali hiyo hutanuka katika nyumba, mtaa, kitongoji, mji, mpaka nchi. Kutokana na hali hiyo, tukawajibika kuweka kanuni na sheria na kuteua wasimamizi wa kuhakikisha sheria za kuhifadhi mazingira zinafuatwa kikamilifu.

Hapo zamani dunia haikua hivi ilivyo, dunia ilikua inavutia inapendeza katika macho ya mwenye kuitazama. Haya tunayoyaona katika uharibifu wa mazingira ni kazi ya mwanadamu akaibomoa na hali yeye mwenye anaishi ndani yake. Kilichobaki ni sisi wenyewe kujilazimisha kuyahifadhi mazingira yetu, tukiendelelea kuyapuuza mazingira haya maisha yetu yatakua hatarini.

Milipuko ya magonjwa, majanga ya mara kwa mara, kuongezeka kwa vifo visivyotarajiwa ni katika matokeo ya kuyapuuza mazingira.

Enyi wanadamu mliojaaliwa akili nawakumbusha kuwa, kama tutayapuuza mazingira yetu basi tutahatarisha maisha yetu.



DustBin
 
Upvote 0
Back
Top Bottom