Uko sahihi! Kama una uchumi mzuri mke wako anapaswa kufanya kazi ya kulea familia tu na sio vinginevyo!
N.B: Mwanamke hajaumbwa kupambana mwanamke ni pamboπ
Kasome vizuri mithali 31 :10-24 uone mke mwema alivyo!!
Uone bibi yako yuleeee was zamani alivyokua!!
Wanawake waliolewa tangy zamani wafanye kazi nyingi sana za uzalishaji na KAZI ya mwanamme ilikua ni kuelekeza kipi sahihi kifanyike na yeye mke afanye sahihi kilichoelekezwa!!
Ulipoingia ushetani wanawake wakawa wavivu eti wao watoe uke ili wahudumiwe yaani biashara ya HUDUMA Kwa UKE kwenye ndoa ndivyo ilivyo Sasa ambavyo ni ushetani!!!
Kuzaa Kwa uchungu na kula Kwa jasho ni laana aliyopewa mwanadamu sio majukumu kama wengi wanavyojitahidi kuhubiri siku hizi ili kuhalalisha biashara haram!!
Nenda kasome uone,jinsi anavyoamka mapema kupalilia mizabibu na kazi kibao Hadi mumewe humuamini!!!
Mithali 31
10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.
12 Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.
13 Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
14 Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.
16 Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.
18 Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.
19 Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.
20 Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22 Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,
29 Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.
31 Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.