Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,943
Twende kwenye mada
Swali 1:Je, leo ukifukuzwa kazi, kusimamishwa au ukiacha kazi ghafla utakuwa katika hali gani?
Je, mshahara kama hutowekewa kwa sababu zozote zile aidha bahati mbaya au kwasababu nyingine utakuwa na afya moyoni? Je, biashara unayoifanya ikianguka ghafla au wewe mwendeshaji ukiumwa kwa miezi 3 mfululizo utakuwa ktk hali gani?
Swali la 2: Kama kuna mtu analipwa na Mwindi 105,000 Tshs kwa mwezi na anatabia ya ulevi, uzinzi au kucheza kamari(bahati nasibu) je, hatachukua sehemu ya ujira wake na kumaliza au kupunguza kiu yake?
Kama lazima atachukua sehemu ya mshahara au posho kutimiza kiu yake basi kuweka akiba inawezekana kwa kila mtu hata mwanafunzi wa chekechea anayepewa 500/= kwa siku kwaajili ya kununua pipi shule ikiwa tu ataweza kuvitambua vitu gani ni muhimu sana ,vitu gani ni muhimu ila sio sana na vitu gani ni anasa (ziada) kwangu.
Kuweka akiba ni jambo muhimu, watu hufedheheka sana kwasababu hawaweki akiba. Wakati wa Rais Magufuli watu wengi wamefedheheka. Mtu kasimamishwa kazi kwasababu ya ufisadi au uzembe sasa anaishi hali ngumu, alisahau kujipangia kile kiasi alichoibia umma kukigawa na kukiweka akiba kwaajili ya kesho.
Hebu tujiongezee mfuko wa jamii wa kibinafsi kwa kuweka fedha kwenye fixed account, kibubu imara cha chuma au kwenye line za simu. Weka kulingana na kipato chako.
Ni aibu jamii inakuheshimu siku moja umekwama unaanza kukopakopa mpaka kwenye vijiwe.
Narudia tena kwakusema usipoweka akiba soon utafedheheka