Kama uko tayari kuingia shamba msimu huu wa kilimo karibu tuunganishe nguvu kazi

Jifunafu

Senior Member
Joined
May 25, 2020
Posts
182
Reaction score
693
Ndugu wanajamvi,

Kama uko tayari kuingia SHAMBA msimu huu wa KILIMO karibu tuunganishe nguvu kazi,twende tukampige mkoloni Kule Katavi.

Kama na wewe uko tayari na unayo nia kutoka moyoni na unachokianzio kidogo karibu tuunge nguvu twende tukalime mahindi katavi msimu huu unaoanza.

Hapa ni kazi kazi naenda kama mwanakijiji wa kawaida na Wala sio kwenda kuzuga.

Maisha haya ukayachekea nayo yanakucheke ni kukaza Buti hadi kieleweke.
 
Muhimu usiingie kwenye kilimo kwa pupa. Hakikisha unataarifa za msingi za mambo yafuatayo:-

1. Zao unaloenda kulima: Hakikisha umejua soko la zao lako, kanuni bora za uzalishaji wa zao lako ukijumuisha na uzoefu kutoka kwa wanakijiji.

2.Ubora wa shamba unaloenda kulima. Tumia historia ya msimu au misimu iliyopita kujua ubora wa shamba utakalonunua au kukodi. Ukienda kichwa kichwa unaweza uziwa/ kukodishiwa shamba kwenye mkondo wa maji au shamba lililochoka sana ukaishia kuwa maskini mara mbili.

3.Gharama za ushalishaji. Takwimu mpya zinaonyesha kwamba Output( Gross Income) kwa mazao mengi inaongezeka lakini Net Income inazidi kupungua kutokana na gharama za uzalishaji kuzidi kuongezeka.
Chagua kulima zao ambalo linaunafuu wa gharama za ushalishaji km Alizeti na karanga ili kutengeneza faida kubwa.

NB: Ukiingia kwenye kilimo kwa umakini unaweza kupata utajiri ila ukiingia kwa pupa kinaweza kukufanya masikini wa kutupa.

Ni ushauri tu.
 
Hapa kwenye Gharama mkuu ndo watu wanalia hasa kama ndo msimu wa kwanza kulima…otherwise They are all valid factor to consider!
 
Muhimu usiingie kwenye kilimo kwa pupa. Hakikisha unataarifa za msingi za mambo yafuatayo:-

1. Zao unaloenda kulima: Hakikisha umejua soko la zao lako, kanuni bora za uzalishaji wa zao lako ukijumuisha na uzoefu kutoka kwa wanakijiji.

2.Ubora wa shamba unaloenda kulima. Tumia historia ya msimu au misimu iliyopita kujua ubora wa shamba utakalonunua au kukodi. Ukienda kichwa kichwa unaweza uziwa/ kukodishiwa shamba kwenye mkondo wa maji au shamba lililochoka sana ukaishia kuwa maskini mara mbili.

3.Gharama za ushalishaji. Takwimu mpya zinaonyesha kwamba Output( Gross Income) kwa mazao mengi inaongezeka lakini Net Income inazidi kupungua kutokana na gharama za uzalishaji kuzidi kuongezeka.
Chagua kulima zao ambalo linaunafuu wa gharama za ushalishaji km Alizeti na karanga ili kutengeneza faida kubwa.

NB: Ukiingia kwenye kilimo kwa umakini unaweza kupata utajiri ila ukiingia kwa pupa kinaweza kukufanya masikini wa kutupa.

Ni ushauri tu.
Mkuu!Hapo kwenye alizeti naomba uongezee nyama katika suala la gharama kuwa ndogo.
 
Back
Top Bottom