Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
#Roadlife_ hints by Thomas B Mwamfupe
Katika kukumbushana tu,unajua kama wewe Trucker ni muwakilishi wa kampuni yako kule unakotumwa kupeleka mzigo, kama hukulijua hili basi ujue toka leo.
Unapotumwa kupeleka mzigo mahali tayari unaiwakilisha kampuni yako huko unakotumwa, hivo huna budi kuwa makini ili uiwakilishe kampuni yako vema,uwakilishi wako mzuri ndo utaifanya kampuni yako ionekane ya maana na pengine kupata mizigo mingine zaidi ya kupeleka.
Jitahidi kufikisha mizigo kwa wakati, na ukifika jitahidi kuwakilisha karatasi mapema mahali husika, ofisini, kuwa na muonekano mzuri kwa maana ya dressing yako na sio unaingia ofisi za watu huku, umevaa car wash kandambili na pens huku umechomeka mswaki, kwenye pens yako na mdomoni kuna mabaki ya povu la Colgate, nk kwa muonekano huo wenyeji wako wataona kama kampuni nzima ndivo mlivo.
Hivyo kuiletea sifa mbaya kampuni, yaani unakuwa rafu wanashindwa hata kuelewa ni vipi umeaminiwa. Huo mzigo, na kama vipi kampuni yako wanatoa uniform basi ni vema ukatupiamo hizo uniforms zako na uka appear smart, kama umepark gari yako ndani ya yard yao halafu ukashusha jiko basi ukishamaliza safisha hapa mahali ulupopatumia na paache pasafi kama ulivopakuta, lakini ile tabia ya umenyonyoa kuku zako wa isoka au Kabanga halafu manyoya unayaacha hapohapo, mabaki ya mkaa, mara maganda ya viazi, yaani uchafu kwa ujumla anaacha pako vururu vururu, unajisikiaje kwanza, kuwa smart, sifa moja kubwa ya trucker ni usafi, jitahidi kuwakilisha vema fani yako, kwani uongooo !!!?
Unaenda mgodini, unajua kabisa unatakiwa kuwa na PPE, unaanza kuunga unga na nguo za kuingilia mgodini, unavaa nguo juu ya nguo zingine, unaazima viatu, hivi hukujua kuwa unaenda mgodini na hujui. Ukiingia mgodini au kushusha/kupakia mafuta hukujua unatakiwa uvae vipi.