Kama ulipitia haya yote basi wewe kwa sasa unatambulika kama muhenga

Deadbody

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
4,274
Reaction score
6,595
UTAJUAJE KAMA WEWE NI MUHENGA?

1. Kama ulikata daftari mara mbili. Kipande kimoja ukaacha nyumbani na kingine ukaenda nacho shule. Wewe ni muhenga.

2. Kama ulitumia kipande cha kandambili kama ufutio.

3. Kama ulikanyagia kisigino ulipotoka kuoga ili usichafuke kwa kuwa hauna kandambili....Wewe ni muhenga.

4. Kama kwenu mlianika betri za national ili ziongezeke chaji kwenu..... Wewe ni muhenga.

5.Kama ulilala na sare za shule ili asubuhi usichelewe halafu asubuhi ukajikuta umejikojolea Wewe ni muhenga.

6. Kama ulienda choo porini na ukajipangusa kwa nyasi hongera aisee.....We ni muhenga

7. Kama uliweka chumvi kwenye uji mweupe ndio ukanywa....Wewe ni muhenga

8. Kama ulilamba sukari ukapangusa mikono na ukasahau mdomo....sema kichapo heheeee..Wewe ni muhenga

9.Kama uliogea karai la chuma Wewe ni muhenga

10.Kama uliambiwa ushike sikio la kulia kwa kupitisha mkono wa kushoto juu ya kichwa ndio uende darasa la kwanza.....Wewe ni muhenga

11.Kama ulipaka mafuta yanaitwa RAYS ya bluu au YOLANDA....Wewe ni muhenga

12.Kama sare yako ya shule ilikuwa na viraka vingi hadi watu wasitambue rangi ya sare ya shule yenu.....Wewe ni muhenga

13.Kama ulivalishwa nepi na sio papmpers.....Wewe ni muhenga

14.Kama ulikunywa maji kwa kata na ukaogea sabuni ya REXONA. Wewe ni muhenga

15.Kama wewe ni mwanamke na Uliwahi kuvaa viatu vya LOSO Wewe ni muhenga.

16. Kama ulipenya njaa ya mwaka 1984 na bado unaijua facebook Wewe ni muhenga.

17.Kama ulipakwa Gv au mafuta ya breki ya AGIP kwenye kidonda.....Wewe ni muhenga

18.Kama ulienda shule peku huku umebeba kuni na maji ya kuwapikia walimu..Wewe ni muhenga

19.Kama ulivaa kandambili mikononi wakati mnacheza mpira wa makaratasi "one touch".....Wewe ni muhenga

20.Kama uliweka kioo chini ya dawati ili uwachungulie wasichana...Wewe ni muhenga

21.Kama mpiga picha alishakuambia picha yako imeungua basi wewe pia ni muhenga

22.Kama wewe ni msichana na uliwahi kuvaa NYANYAPUZO Wewe ni muhenga

23.Kama uliwahi kutengeneza magari ya waya,mabox na makopo yalioisha KIMBO Wewe ni muhenga

24.Kama uliwahi kucheza ule mchezo wa kifimbo cheza Wewe ni muhenga

25.Kama ulitumia GUNZI kuchambia au kujisugua makalio chini Wewe ni muhenga

26.Kama ulienda shule na sukari kwenye kipande cha gazeti kwa ajiri ya kuweka kwenye bulga Wewe ni muhenga

27.Kama uliwahi kuvaa ndala za SKY WAY ,NODIN,UMOJA na viatu vya bora Wewe ni muhenga

28.Kama uliwahi kukojoa dirishani kisa unaogopa kutka nje Wewe ni muhenga

29.Kama uliwahi kuogea sabuni ya komoa,komesha,mshindi,ilula Wewe ni muhenga

30.Kama uliwahi kutumia TANBOND,KIMBO,,,,Wewe ni muhenga

Hebu waite wahenga wenzio uliocheza nao
 
Mi muhenda wa mengi kati ya hayo , lkn ni muhenda zaidi wa kuchelewa kurudi shule muda wa mapumziko na huambulia bakora
 
Kama ulivaa soksi za pundamilia pia wewe n mhenga tena ulieshiriki kutunga methali zaman
 
Kama ulikuwa ukitumia togwa
Kama ulivaa laizoni
Kama uliendesha Phoenix au swala
Kama ulikula ugali wa mtama na ngulu
Kama ulitumia bwimbwi na pepeta
Kama ulitumia shilingi kumi ya noti, ishirini, na ishirini na tano ya gwala
Kama uliwahi kuingia katika kibisa
Kama ulikuwepo kipindi jeneza likipita jirani na kwenu unakimbia na kujificha ndani
Kama ulikuwa ukisikiliza kipindi cha pwagu na pwaguzi au juma na uledi
Kama uliwahi panda yale mabasi ya kusafiri usiku
Kama uliwahi panda punda kama usafiri
Kama uliwahi kula mahindi na maboga kama chai
Asee wewe ni MUHENGA
 
Kama ulienda kuwinda swala, sungura ngedere kutumia mbwa na kombeo wewe ni muhenga.
Kama uliwahi kumwandikia mpenzi wako barua kutumia karatasi ya daftari, ukaweka poda, wewe ni muhenga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…