Kichwa cha habari kipo katika kukuamsha wewe ndugu, rafiki, jamaa, mzee, kuwa Yesu yupo malangoni kuja kulichukuwa kanisa,
Tupo karibu sana, na ile dhiki kuu, mpinga Kristo anasafishiwa njia sasa, dalili iliyo kuu ni hii!
kuwapumbaza watu makanisani kupitia harufu mbaya inayo chafua uwepo wa Roho mtakatifu katika watu, moja ya uchafu wa kiroho ni AI - Artificial Intelligence hasa katika matumizi ya nyimbo,movie na mafundisho yanayojinasibisha kuwa ni ya Mungu kumbe yanatoka kuzimu.
Kupitia Ai, wahubiri hawahubiri tena, kupitia Ai, waimbaji hawaendi tena studio, pia mafundisho mengi yanatokana na Ai na si Roho mtakatifu,
Kila mtu na atafakari, Ai imekuja kuuwa nguvu ya Roho mtakatifu kwa watu, maana watu watategemea Ai kwa mambo mengi zaidi kuliko hata kuomba ili wapate yaliyo ya Mungu.
Ai ni kiungo cha mpinga Kristo, japo imekuja kama inamsaada, lakini ni njia ya kuzimu na matokeo yake ni kukataliwa na Mungu.
Hivyo basi, Linda sana moyo wako maana huko, ndipo chemchem za uzima, zinapo toka.