KAMA ULIZALIWA BAADA YA MWAKA 1995 HAYA MAMBO MENGI YALIKUPITA

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,904
Reaction score
4,902
1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa jumapili tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili' a.k.a tetesakrin
5. Kupamba kadi na pamba sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa kwa mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Wavulana kuvaa nguo ya ndani aina moja nchi nzima (VIP), usiombe ikakatika ukakuta imebana kifua.
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Nchi nzima Kuangalia Movie ya Commando John, Double Impact, Rambo na Bruce Lee..
12. Watoto Wa Mtaa Mzima Kufahamiana sababu ya kucheza Wote Jioni Kombolela na Kibaba..
13. Kuunguzana na tunda ya Ubuyu baada ya kulisugua chini
14. Kukata ndala, eti ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16. Kuweka Vibox box kwenye Shati la shule Mgongoni..
17. Kuweka Shati la Shule "Blue" eti liwe maridadi.
18. Ubitozi Ulikuwa ni Kusimamisha Kola Ya Shati.
19. Ukiandika Barua kwa Umpendae lazima uchore moyo na Mkuki na lazima upulizie Pafyumu ya "YU".

20. Hata kama Mlikuwa mmegombana January lakini Mtu anakwambia ngoja shule ikifungwa

#WeweUnakumbukaIpi
#Share
 
-Kukunja daftari na kuweka mfuko wa nyuma.
-Darasani kuwawekea wadada tuvioo ilikuona nguo za ndani
 
Nimecheka,hasa hapo kwenye double impact.Umesahau bollo young,Commando suzy,charle mnene na charle mwembamba.
Mimi nakumbuka kucheza UKIMWI na upiiiiiiiite,kucheza rede kujaza chupa mchana,kuruka kamba.
Kuandika barua lazima useme mimi ni mzima ,sijui wewe ulie mbali na upeo wa macho yangu.
Mifuko ya Rambo ile ya mistari mistari kubebea Daftari.
 
ukienda kuoga unazisugua ndala zako za skyway mpaka zinakua mpya,
Umenikumbusha Losso,nilikuwa darasa la vidudu nilikuwa natamani nivae nikiwaona mama zangu wadogo wametinga Losso za pinki
 
1.Mpira wa makaratasi,
2.kuogelea mtoni na kuvua vichwa runguu,
3.kutoboa toboa na vijiti mgomba wenye ndizi mbivu ili tuzile,
4. kombolela,
5. vita ya matope,
6.kwenda kutega kanga.
7.Kuweka mitarakwe ndani siku ya krismasi.
Dah vipo vingi sana enzi hizo miaka ya 1997/98.
 
Hapo pa kung'olewa jino kwa uzi simsahau my kaka unyama alonifanyia[emoji134][emoji134][emoji134]

Alikuwa na kawaida ya kunifunga uzi kwenye jino then ananiacha nao nakuwa nauvuta taratibu kulegeza jino hadi litakapong'oka. Sasa siku hiyo kanifunga uzi vizuriii kumbe kaufunga kwenye jiwe kubwa, ile nanyanyuka na jino likang'oka. Haki nililiaaaaa.
 
1.kucheza Kula mbakishie baba
2. Kucheza mpira wa visoda
3. Kucheza ukuti ukuti
4. Kucheza mdako
 
Yan umenikumbusha mbali we dada.
Hakuna mchezo ulikuwa unanimaliza akili kama ukimwi

Na dama aka malaiti hahahahaahah

Yan we utakuwa mhenga wa rika langu

Loso nayo ilikuwa ni habari nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…