Kama Umeme hautoshi tunajadili PPP ya Msambazaji ili Asambaze nini ?

Kama Umeme hautoshi tunajadili PPP ya Msambazaji ili Asambaze nini ?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Tuliambiwa umeme hautoshi ndio maana kukawa na Mgao, tunaambiwa hata Bwawa likiwa full Capacity (mara mbili ya uzalishaji wa sasa) bado bei hazitashuka sababu kuna mahitaji makubwa ya viwanda n.k.

Sasa najiuliza hawa Adani na wengineo ambao eti wameleta ombi la kufanya usambazaji, wanasambaza nini na wapi ? Pili kuongeza mtu kati lazima na yeye atachukua chake hivyo kugawana faida na kama ni hasara sisi Wabia wake ndio tutafidia Hasara ili apate faida...

Binafsi nilishauri Tanesco aingie UBIA ila aingie kwenye vitu ambavyo hawezi kufanya au mpaka sasa hafanyi au hana expertise ya kufanya....


Pili nilishauri kila mtu anayeweza aingie UBIA na TANESCO katika uzalishaji, tena nilisema sio raia kutoka nje (sababu tuna vyanzo na uwezo wa kuzalisha Gigawatts za kutosha); bali kila raia awe mzalishaji na azalishe kutumia solar na kuwauzia TANESCO kama Credit...; na kama wewe una mbinu yako ya kuzalisha ambayo itakuwa gharama nafuu kuliko vyanzo vya TANESCO (hydro, gesi n.k.) basi watanunua kutoka kwako na kuuza kwetu na wabakie na chenji ya kufanyia ukarabati


Tusifanye Kosa la kugawa urithi wetu, tunajua yaliyotokea huko nyuma, pia kuingia UBIA tuingia jambo ambalo hatuwezi kufanya au tuache wigo wa watu binafsi kushindana kutupa Huduma, sio kuingia UBIA kwenye vitu ambavyo ni Naturally Monopoly na watu hawana choice bali kutumia huduma husika...; UK walifanya haya na sasa wanajuta kwa bei kuwa inflated bila uhalisia...

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichonacho, Tufanye Tunachoweza
 
If we Pay for it..., we Should Own it....
 
Back
Top Bottom