Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Uchawi hauitaji details, uchawi unataka sababu tu mtu akipata sababu hata ya kukusababishia unakwenda na maji. Anaweza akaja kukuomba chumvi kile kitendo cha kumnyima tu ni sababu tosha, '' ''tunayaweza yote katika yeye atutiaye nguvu''.
Kweli mkuu nakumbuka kuna nyumba niliwahi kupanga asa kuna siku Mwenye nyumba alipiga floor Kwa nje me sikujua ile naingia tuu nikakanyaga halafu ilikua mbichi, ebhana Yule mbaba alichonifanyia usiku sitosahau yaani ile alichukulia ni 7bu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukinywa pombe za moshi ni kawaida kuona mavitu ya namna hio huko vijijini.
Hakuna cha mwanga wala jini.
Gongo nuksi

.
 
Angekuwa na uwezo huo angekuwa anakesha humu JF kupiga Porojo?
Acheni imani za kishirikina. Mtaliwa hela kilaini na wajanja.

.
 
Ukipata tatizo watafute hao watu. Wana Mungu wale [/QUOTE]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka wkt fulani nyuma jamaa alikamatwa sikumbuki mkoa
Alikuwa anaingia kichawi nyumba za watu na kuwaingilia wanawake,haijalishi umeolewa au la,yeye anakula mzigo,ikaenea hiyo taarifa,siku ya siku akaingia nyumba ya mtu akanasa mpk asubuhi,kupigwa akasema kuwa ni yeye ndio alikuwa anawaingilia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulikuwa unasoma huko au ndo nyumbani?
 
Hii imetokea mwaka jana kuna kijiji uko kwimba mwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchawi upo.....Mwezi jana mzee masumbuko huko wilayani makete ikonda wananzengo wamemtimua jamaa kwa kuwaingilia raia...Alilamba mke wa mwenyekiti wa kijiji na diwani viti maalumu na wananzengo kibao wakike na kiume.......Uchawi upo Umelala na mkeo kumbe mdau anafaidi huna habari na mbaya zaidi akikukula anatangaza mtaani jinsi ulivyo daaaah! siku ya kikao cha kumtimua wamama walilalamika mpaka huruma aisee.......Eeee Mungu kiponye kizazi changu
 
We nae unazingua kiranga, unashindwa nini muda mwingine kutuacha tufurahie masimulizi kwani lazima uje ukomenti utuharibie siku????

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndiye unazingua.

Unashindwa nini kuniweka ignore list usione kabisa ninachoandika nisikuharibie furaha yako?

Niweke ignore list tu, hutaweza kuona ninachoandika.
 
Wewe ndiye unazingua.

Unashindwa nini kuniweka ignore list usione kabisa ninachoandika nisikuharibie furaha yako?

Niweke ignore list tu, hutaweza kuona ninachoandika.
Tatizo vingine unavyoandika napenda kuvisoma, nikikuweka huko maana yake nitakosa yote naona bora tu nivumilie maudhi, ila muda mwingine unazingua sana boss wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo vingine unavyoandika napenda kuvisoma, nikikuweka huko maana yake nitakosa yote naona bora tu nivumilie maudhi, ila muda mwingine unazingua sana boss wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sitaki nataka.

Ujue, kwa watu waungwana kuna maamuzi mengine magumu.

Kwa mfano, pale unapoona wewe nakuzingua, ndipo mwingine anapoona ananifurahia kabisa.

Na pale unapoona wewe unafurahia, ndipo mwenzako anaona nazingua sana.

Sasa nikikusikiliza wewe, nisiandike usichotaka niandike, halafu nikamsikiliza mwenzako naye, nisiandike asichotaka niandike, nikajikuta wawili nyie mme cancel out kila kitu ninachotaka kuandika, hapo itakuwaje?

Ndiyo maana mimi naona, kitu muhimu ni kuandika ninavyoona sawa, kama nakuchefua uniwie radhi tu.

Kwa sababu kauli mbiu ya JF inatutaka tufunguke kwa uhuru.

Sasa ukianza kunipangia jinsi ya kuandika unakuwa kama huelewi falsafa nzima ya kufunguka kwa uhuru JF.

Kuna mtu kaandika story mbaya sana ambayo kwa wengine inaweza kusemwa ni matusi yasiyostahilika, lakini mimi nikaona ni uhuru wake tu.

Kwa hivyo, naomba univumilie tu.

Ukianza kuniwekea mipaka nitakosa kuwa Kiranga, nitakuwa Kiranga Light, mara Kiranga Diet.

Utakuta hata yale unayoyapenda kwangu wengine wameyachakachua kwa censorship kama wewe.

Mwisho kila mtu atamkataza mwingine kuandika lolote.

Ba JF itakufa.
 
Duh, umeniandikia gazeti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…