Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Wangemla na yeye
 
Walilalamika?
Kwanini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitasahau siku moja mwaka 2002 nikiwa nasoma NJOMBE Shule ya msingi X.. Mida ya mchana mchana niliomba ruhusa kwa mwalimu akaniruhusu kwenda chooni kila chumba cha choo kilikua na mtu mzma wa makamo tena mmoja yuleyule kila chumba.. Nilikimbia mbio kwa uoga. Nilimweleza mwalimu tukatoka nje na wanafunzi wengine wakaingia lakini walidai hawakuona chochote.. ilitolewa amri kwenda chooni kwa vikundi. SITASAHAU
 
Nakumbuka 2006 niliugua Sana kichwa huku nikihisi baridi Kali Kama ile ya malaria. Wazazi wangu walizunguka na Mimi hospitali nyingi tu lakini kila wakipima hawaoni ugonjwa lakini Hali yangu Ni mbaya kwelikweli.
Kama hujawahi kuuguliwa huwezi kwenda Kienyeji maana Hakuna utachokifata. Wazazi wangu waliamua kunirudisha nyumbani lakini hali ilivyozidi kuwa mbaya wakaamua kunipeleka gereji. Gereji ya Kwanza fundi alifeli, kesho yake tukaenda gereji nyingine fundi Ni mama wa makamo. Alileta spana zake akaanza kazi, aisee nilipona hapohapo nikawa mzima.
Mpaka Sasa naamini ushirikina upo bila msaada wa Mungu kupitia yule Mmama wangenipoteza.
 
Mganga wa kienyeji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kajumanne amaizing hivi hakuna karaha wala nini. Kama kawaida yangu hupenda kufukua mambo yasiyopendwa kuongelewa sana humu ila ndo yanayofanyika sana kwenye jamii zetu.
  • Je, umejizindika? Una kinga ya kutosha maana yule jamaa sio mchezo.
  • Hii gari ukiiba utarudisha mwenyewe
  • Mimi atakayejaribu kuniroga aandae kaburi tu, mimi sijaribiwi kabisa. Kwetu nimeaga ukijaribu unakwenda na maji.
  • Ninalindwa na mizimu atakayejaribu atashindwa hapa vinadunda tu.
  • Hii biashara yangu watu waliichezea sana nilipozindika tu sahv biashara inaenda vizuri mwanzo hela zilikua zinapotea tu dukani.
  • Nimezindika biashara yangu dhidi ya chumaulete. Sasa na wewe utafanyaje biashara kienyeji enyeji tu hapa mjini bila kuizindika na wewe? Unawajua waswahili wewe au unawasikia? Siri ya mafanikio biashara lazima uzizindike bila hivyo hakuna utakachokifanya.
Hayo ni maneno ya watu wengi I mean maneno ya mtaani na watu kuhusu suala la kujizindika au kuzindika biashara.

Swali kwa wewe mwanaJF mwenzangu:

Je na wewe umejizindika? Au unaishi kienyeji kama mimi tu? Tuseme ukweli!
Je, nyie wenye biashara humu tusaidianeje? Umezindika biashara yako hapa mjini?
Je, dhana ya kuzindika biashara ipo?
Usipozindika biashara je?
Je, ni kweli biashara hapa mjini bila hata kamzizi au jani haziendi?
Ushawahi kuexprince nini kuhusu haya mambo?

Nitakuja kuwapa kisa kimoja hivi soon.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…