Kama umeweka hela kwenye VICOBA nenda katoe

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Wanajamvi natoa ushauri tu!

Kama umeweka hela kwenye Vicoba nenda katoe.

Nawapa sababu.

Corona ni tishio na ndio hivyo vitu vimeanza kupanda bei kutokana na uzalishaji finyu na uhitaji mkubwa, low supply lakini high demand, hapo kunatokea shortage ambayo inalazimisha watu kupandisha bei ili kuifikia equilibrium 'Cobb web'

Kwa sababu hii hela nyingi itatakiwa kukimbizana na bidhaa kidogo, ndipo kwenye maana ya mfumuko wa bei, kutokana na shughuli nyingi kukwama itakuwa ngumu mtu awe anaiangalia hela halafu afe njaa.

Sasa ili kuepusha ugomvi wa kwenye vicoba na vitu vingine vya kufafana na hivyo kachukue hela zako, ukaweke mwenyewe benki ili kama ukila ule mwenyewe, au uzitumie kuweka stock kidogo nyumbani kwako maana mambo yanazidi kuharibika.

Ni ushauri tu! Sio lazima

Kuna muda nitakuja kushauri zaidi kuhusu Hisa, na uwekezaji mwingine kwenye masoko ya pesa.

Kwa wale wenye pesa benki muda bado, nitawashauri kitu nikiona viashiria vya hatari.

Signed

Oedipus
 
Mambo yameanza kwenda kombo
Tutaikubali tuu hiyo chanjo, Hatuwezi kuukwepa huu Ukoloni Mambo Leo
 
Benki nao wakizidiwa hawali hela..??
Tukikaribia anguko la uchumi jua itakula kwetu, ndio maana nimesema nitasema kuhusu hayo nikiona baadhi ya vitu

Ila vicoba vingi sio safe ukilinganisha na benki
 
Bora kuchomoa pesa
 
Bora kuchomoa pesa
Ukianza kutoa hela sasa, kuna majanga kidogo kwa hizo taasisi, zitaishiwa ukwasi na wanaweza kufunga.

Bado uchumi hauko vibaya kwa benki, ila hawa vicoba ambao kesi za kudhurumiana ni nyingi, hali imeshaanza kubana kwa hiyo kudhulumiana kutaongezeka, thus nimeanza nao
 
mmh!
Ngoja nimpigie Mama Winnie aniandalie hela yangu kabisaaa, jioni nitaipitia kumbe ndio hiyvo!
 
Wanajamvi natoa ushauri tu!

Kama umeweka hela kwenye Vicoba nenda katoe.

Nawapa sababu.

Corona ni tishio na ndio hivyo vitu vimeanza kupanda bei kutokana na uzalishaji finyu na uhitaji mkubwa, low supply lakini high demand, hapo kunatokea shortage ambayo inalazimisha watu kupandisha bei ili kuifikia equilibrium 'Cobb web'

Kwa sababu hii hela nyingi itatakiwa kukimbizana na bidhaa kidogo, ndipo kwenye maana ya mfumuko wa bei, kutokana na shughuli nyingi kukwama itakuwa ngumu mtu awe anaiangalia hela halafu afe njaa.

Sasa ili kuepusha ugomvi wa kwenye vicoba na vitu vingine vya kufafana na hivyo kachukue hela zako, ukaweke mwenyewe benki ili kama ukila ule mwenyewe, au uzitumie kuweka stock kidogo nyumbani kwako maana mambo yanazidi kuharibika.

Ni ushauri tu! Sio lazima

Kuna muda nitakuja kushauri zaidi kuhusu Hisa, na uwekezaji mwingine kwenye masoko ya pesa.

Kwa wale wenye pesa benki muda bado, nitawashauri kitu nikiona viashiria vya hatari.

Signed

Oedipus
Umeongea jambo la msingi sana mkuu hasa kwa wakt huu, mawaza ata kutoa visenti vyangu benk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: OLS
Back
Top Bottom