Kama una alama hizi 14 wewe ni mke bora kwenye sayari ya dunia

Kama una alama hizi 14 wewe ni mke bora kwenye sayari ya dunia

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Kuwa mke sio kazi rahisi, khususan kuwa mke bora na sio bora mke. Lakini, iwapo unafanya mambo haya 14, kuna nafasi kubwa mumeo anajua kwamba ana mke bora kwenye uso huu wa dunia.

1. UNAFURAHIA MAFANIKIO YAKE

Amepandishwa cheo kazini, amemaliza masomo yake, au amefanikiwa kufanya jambo fulani zuri. Anapokuwa anafurahia mafanikio ya jambo fulani, nawe unafurahia pia. Utakuwa mke maridhawa kama utayachukulia mafanikio ya mumeo kama ya kwako na ukayafurahia.

2. KUPENDA ANACHOKIPENDA

Kuna kitu anachokipenda, japokuwa hakikusisimui, lakini wakipenda kwa sababu mumeo anakipenda na kukihusudu.

3. UNAMUWEKA MBELE

Yeye ni nambari 1. Unahakikisha kwamba kazi na mapendeleo yako sio muhimu kuliko yeye. Hakuna yeyote ambaye ana kipaumbele cha juu, si marafiki zako, familia hata watoto.

4. UNAPENDA KUFANYA VITU MWENYEWE

Kwa kuwa yeye ni kipaumbele chako, unajitahidi kadiri uwezavyo kuhakikisha kuwa wewe ndiye unayemhudumia badala ya watu wengine. Unapenda kumpikia, badala ya kuacha kazi hizo mikononi mwa mfanyakazi au watu wengine.

5. UNAMPIKIA CHAKULA ANACHOKIPENDA

Unampikia chakula anachokipenda ili kumuonesha kwamba unajua anachokipenda na unataka kumfanyia vitu vizuri.

6. UNAMFANYA ACHEKE

Utakuwa mke bora duniani kama unayajua mambo yanayomfurahisha na unajua kitu gani kinachomchekesha na kumfanya atabasamu.

7. UNATUNZA SIRI ZAKE

Iwapo mumeo hapendi na hatafurahia hatua yako ya kusema jambo fulani kwa mtu yeyote, hutalifanya. Wala hutasema lolote kuhusu jambo hilo kwa mama yako au mtu yeyote unayekutana naye. Mume anakushirikisha mawazo yake binafsi kwa sababu anajua kwamba anaweza kukuamini.

8. UNAWAPENDA ANAOWAPENDA (NAO WANAKUPENDA)

Yumkini mumeo alikuwa na marafiki wema kabla ya ujio wako, hivyo ni watu muhimu ambao wamechangia kumtengeneza mumeo. Unashukuru kwa kuwa na watu wa aina hiyo katika maisha yenu, na hujali pindi anapotaka kuzungumza nao kwa muda fulani.
Hivyo, kama marafiki zake wanakupenda, hiyo ni alama ya uhakika kwamba wewe ni mke bora.

9. UNAMRUHUSU AKUFANYIE VITU

Miongoni mwa mambo muhimu unayotakiwa kuyajua ni kwamba, wanaume wanahitaji kuhisi kwamba wanahitajika, na mke bora humruhusu mumewe amhudumie.

10. UNAMPA TAARIFA

Mke bora huhakikisha anamfanya mumewe ajue kuwa anampenda. Hata kama unachofanya ni kumtumia sms, unapohakikisha unamwambia “Ninakupenda” kila siku na bila kuchoka, bila shaka utakuwa mmoja wa wake bora duniani.

11. HUMSUMBUI

Ni kweli kwamba unataka awe mtu bora kabisa, lakini unatambua kuwa wewe sio mama yake. Badala yake, nyinyi ni washirika mnaojaribu kusaidiana kuboresha mambo. Unajua kumnanga kuhusu makosa yake au mambo unayotaka ayafanye haimsaidii yeye kuwa mume bora au wewe kuwa mke bora.

12. UNAMUOMBEA DUA

Licha ya mambo mengi uliyonayo kichwani, unahakikisha unaongea na Mwenyezi Mungu kuhusu mumeo. Unamuombea apate baraka na afanikishe matarajio yake. Kitendo hiki kinaimarisha uhusiano wa ndoa yenu kila siku.

13. UNATHAMINI MUDA WA KUKAA NAYE

Mnapokuwa pamoja, unamakinika na unaachana na mambo ya kupekua simu yako kuangalia status za Facebook au kujaribu kufanya mambo mengine yanayoondoa umakini wako kwake. Unaufurahia muda wenu wa pamoja na kuhakikisha kuwa unaachana na mambo yasiyokuwa na ulazima.

14. UNAPENDA SULUHU, KWA VYOVYOTE

#Uamuzi ni mbegu
Nyote mnafanya makosa, madogo na hata makubwa. Mnaweza hata mkakasirikiana. Lakini mke bora hupenda suluhu na kutoyapa nafasi makosa hayo, yawe madogo au makubwa.
 
Humu tu
Screenshot_20250226-142049.png
 
Back
Top Bottom