Kama una ndoto endelea kulala, kama una malengo pambania

Kama una ndoto endelea kulala, kama una malengo pambania

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Ni matumaini yangu u mzima na afya tele.

Leo ningependa kugusia na kuongelea kwa uchache mada inayohusisha mafanikio moja kwa moja kwa vijana ni matumaini yangu bandiko hili halitoondolewa au kuunganishwa na thread za awali.

Unajua waarabu wanakamsemo "anniatu min qalbi" kwamba kila kitu ni adhma au nia hauwezi kuota ikiwa bado haujalala na waswali hawakutuacha mbali wakisema "mtaka cha uvunguni shariti uiname" ni kwamba kama umedhamiria kufanikiwa na kuyafikia malengo basi ni sharti ujitambue na utambulike.

KUJITAMBUA
Binadamu unatakiwa kujitambua;
  1. Wewe ni nani?
  2. Unataka nini?
  3. Unafanya nini?
  4. Kwanini umezungukwa na watu hao ulionao?
  5. Tabia zako ni rafiki kwa malengo yako?
  6. Mazingira unayoishi na linanisha kwa malengo yako.
  7. Subra hauwezi kufanikiwa kwa usiku mmoja labda ukatoe kafara ya damu.

KUTAMBULIKA
Ukijimbua ni lazima utambulike kwa watu ni mfano wa mwanasiasa Mh JAKAYA M KIKWETE miaka kadhaa kwamba ya kuiongoza Tanzania katika gurudumu la maendeleo, kumbukumbu inaniambia aliangushwa katika uchaguzi wa ndani mwaka 1995 dhidi ya mgombea mwenza BENJAMINI MKAPA ila haikumpa shaka kabisa ila alijisubirisha kufikia malengo yake kwa baraka zake mungu alifan ikiwa mwaka 2005 na kuwa Rais wa awamu 4.ila nakwambia Usiwe kama lipumba na DR SLAA wote ni wasomi ila hawajitambui ni kwamba hawajajua sababu nilizozitaja hapo juu.

Namalizia kwa kutilia mkazo subira na mikakati ni watoto wa baba mmoja ambae ni mafanikio jitahidi sana kuwa na mipango midogo itakayokufikisha katika hatua yako kubwa.

#JITAMBUE#UTAMBULIKE
 
Back
Top Bottom