Kama una roho ndogo ukiisoma hii barua ya dogo Aslay lazima chozi lidondoke

Kama una roho ndogo ukiisoma hii barua ya dogo Aslay lazima chozi lidondoke

kamati ya ufundi

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
416
Reaction score
439
BARUA KWA MAMA.

Jina langu ni Aslay Isihack, jina hili alinipa Mama yangu mwenyewe Bi. Mozza kutokana na maisha niliyopita ya Muziki wengi wananifahamu kwa jina la Aslay.

Barua kwa Mama yangu kipenzi pamoja na mashabiki zangu.

Hellow Mama najua unanisikia mwanao tangu uondoke life its so complicated kuliko nilivyodhania, kila kitu kwangu tabu nakosa sana ushauri wako natamani kuongea nawe japo hata siku moja lakini nafahamu kwa mapenzi ya Mola haiwezekani nakuombea kila la heri huko ulipo.

Japo kwasasa nimepata kibinti pacha wako, jina lake nimemuita Mozza I wish ungemuona mmefanana sana. Kuna kitu Mama nataka kukugusia juu ya ndoto yangu bado sana natamani kuwa msanii mkubwa kama Kaka zangu na Dada zangu walionitangulia kwenye Muziki. Ndoto niliyokuwa nakusimulia kila wakati tukila Chakula cha jioni.

Mama Kila kukicha Wananirushia mawe nisifike niendapo. Mawe yote Mama nimeyaokota najengea barabara nifike niendapo, hakuna wakunifuta mimi machozi yangu nalia kilio cha mtu mzima maumivu ndani kwa ndani.

Juzi nilitamani nikupigie simu nikuambie yanayonisibu mwanao, Namba yako haipatikani labda umeweka call busy unaniombea dua njema. Nimuambie nani yanayonisibu ndani ya Moyo wangu juu ya Mziki wangu na maisha yangu?

Mashabiki wangu ndiyo wananipa Ujasiri wa kupambana na kukomaa hivo hivo. Sikufaidika na kile nilichokifanya kwa zaidi ya miaka 15
Hata mimi ukiniuliza ilikuwaje nakosa cha kukujibu Mama nataka tukae kikao cha dharura, tuone ilikuwaje.

I feel inferior, najihisi mnyonge, Nawaza nitaanzia wapi?. I just feel hopless and more hopeless day by day. I dont know. Kila ninaposhika panageuka mwiba mchungu kwangu.
Natamani kujua kama unafahamu nanyanyaswa kisa Muziki wangu .

Kiukweli Mama siwezi kulalamika sanaa maana hata wakati napokuwa mpweke mashabiki zangu huniliwaza kwa kusapoti kazi zangu wamekuwa ndiyo faraja kwangu.

Ndiyo wananifanya niwe jasiri wa kuwatengenezea Muziki mzuri kila kukicha. Sometimes nikiwaza mwanangu ataishije, na familia nitaitunza vipi, bila Muziki?

Natumaini utanijibu basi hata ndotoni Mama kama barua yangu utaipokea.

Nimekukumbuka sana mwanao
Aslay.
Nakupenda Mama.
 
Mungu akuinue katika mapito yako mdogo wangu, wewe ni mwanamziki mkubwa sasa, umevuka vikwazo vingi mpaka kufika hapo. Changamoto zipo kila kukicha, Muombe Mungu pambana
 
Badala ya kutengeneza social conscious song, unaenda kuandika online!

Hapa ndipo mwenzenu Chibu anawapiga bao halafu mnasingizia kurogwa au kupigwa vita kumbe mmekosa uelewa wa tasnia!

Yale ya kwenye SIKOMI (wimbo) si yanafanana na haya ingawaje yake ni upande wa mapenzi?!

Lakini mwenzenu badala ya kuwaandikia mashabiki for free, akatengenezea track na huko Youtube inakimbiza kuliko alivyotarajia!



8.1 Million View na wakati anaitoa wala hakuipa backup!​
 
Kitakwimu watu maarufu are very likely kujiua kuliko wasio maarufu kwakua mtu maarufu hua anaamini anapendwa ila hakuna anayemuonyesha affection directly, hivyo hujikuta anaonyesha feelings zake kwa watu ambao hawajali au hawato-love him back.

Hapo ndiyo depression huja, bad case scenario ni kuanza kutumia vilevi Houston, Ray C, Chidi & co worst case ni suicide.
 
Hata kuandika jina lake hajui, eti Isihack. Hiki kijamaa nacho kina swaga za Muumini Mwinjuma.
 
Siku hizi kumbe mpaka wafu wanapita humu Jf!? au mamaake alizikwa na smartphone!? kweli aslay alimzika mamaake kidigitali!
 
Back
Top Bottom