Kama unampenda utamlinda

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
WAPENZI WAKIWA KWENYE PIKIPIKI

Msichana:mpenzi punguza mwendo hii ni hatari jamani.
Mvulana:usijali mpenzi mi naona mwendo uko poa tu.
Msichana:simamishaaaaaaa pikipikipi mpenzi.
Mvulana:Nikumbatie mpenzi.
Msichana:nimekukumbatia mpenzi.
Mvulana:niambie unanipenda kweli?
Msichana:nakupenda sana mpenzi ila punguza mwendo.
Mvulana:naomba vua helment yangu ujiwekee kichwani mwako nahisi joto sana,vaa wewe.
Msichana:nimevaa mpenzi.


Siku ya pili vichwa vya magazeti.
Ajali ya pikipiki imetokea,kulikuwa na wapenzi wawili kwenye pikipiki,kumbe pikipiki ilikuwa na matatizo ya breki, breki zikakataa na pikipiki ikatoka nje ya barabara na kugonga jengo.Akafa mvulana na msichana yuko salama.
Nini hasa kilitokea?
Boyfriend aligundua kwamba breki za pikipiki zimegoma,hakutaka kumwambia girlfriend wake mana angeshtuka ndo mana akampa helment yake ili aweze kupona,halafu akamwambia amkumbatie ila msichana hakujua kwamba anamkubatia kwa mara ya mwisho.

Ujumbe:Ukiwa na mapenzi ya kweli utamlinda yule akupendaye ili asidhurike.
 
Napita tu hapa nimetoka kucheki gemu.man u wametandikwa kama vya binadamu mpaka raha.
MP.
 
loh aibu.....mie siwezi mlinda hivyo bana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…