Kama unaujua wimbo huu na uliuimba shuleni utakuwa na wajukuu!

Shoctopus

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
3,434
Reaction score
1,985
Aaa, eee, iiii, ooo, uuuuuuu!
Hiiiiizi ni herufi kuuu!
Tamka kwa sauti kuuu!
Hiiiiizi a, e, i, o, uuuuuuu!

a, jogoo a, a, aaaaa!
kama jicho e, e, e!
mwenye mpira i, i, iiiiii
o, ni pete o, o, oooo!

u, kikombe u, u, uuuuuuu!
Tazameni nyote juuu!
Tamka kwa sauti kuu,
Hiiiiizi a, e, i, o, uuuuuuu!

Niliuimba sana nikiwa darasa la (i) pale Vinghawe.
 
Kwahiyo wewe unawajukuu? Hiyo nyimbo niliimba sana miaka ya 2002
 
Tuliimba tulipokuwa "vidudu"(chekechea)

Ila hata leo bado wanaimba, haiusiani na kuwa na wajukuu.

Labda kama wewe ulianza "vidudu" ukiwa na miaka 20.
 
Sikuwahi kuuimba, pengine mwalimu wetu alikuwa haujui, ila nakumbuka kuusikia nikiwa nimeshavuka darasa la kwanza. Ni siku nyingi, na ningeamua kukatisha masomo, pengine ningekuwa na wajukuu sasa.
 
[emoji23] [emoji23] dada yangu huyo...
sawa,kuna jamaa anaitwa Riss unamfahamu?mnafanana jina,
alikuwa mwanangu sana,nilifahamiana nae enzi za BBM,kipindi hicho simu janja tunamiliki wachache sana...
 
Hata darasa la kwanza wa mwakani wataimba bado!
 
Inategemea na shule, kama wanaofundisha LA 1 ni walimu wa kizamani basi hadi leo utakuwa unaimbwa
 
Nilidhani mkazo sasa uko kwenye ngonjera na
Tuliimba tulipokuwa "vidudu"(chekechea)

Ila hata leo bado wanaimba, haiusiani na kuwa na wajukuu.

Labda kama wewe ulianza "vidudu" ukiwa na miaka 20.
Hahahaaaa!
 
2002 shule ya mkovanda huko rombo
 
Mmmh je wa kakuku ka mamam rhoda huu tumeimba utoton enzi zileee za miaka 70 na tuliukuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…