Wana jamii nadhani mko poa.
Leo kuna nataka kusema maneno machache sana yenye faida kubwa sana.
Ndugu zangu kama tunatafuta furaha za kweli hapa duniani ebu tujaribu kusaidia wasio jiweza kwa namna yeyote ile iwayo kwani kufanya hivyo kuna manufaaa kwako ww unaesaidia licha ya yule unaemsaidia kufurahi sana.
Nilikuwa na jiran yangu hapa mtaani yeye katika harakati zake akapata ugonjwa akajiuguza sana mwisho wa siku akarudi kwa mola wake. Huku nyuma kaacha mke na watoto wawili ni huzuni sana mana mke wake alikuwa tu domestic servant.
Muda ukaenda nikaona kama wanayumba hivi mana mtu mzima sio mpaka uambiwe kitu. Basi nikajiongeza nikawa nampa mama yake kila wiki hela ya nauli ya shule kwa wiki nzima, mana mtoto anaesoma ni mmoja na mwingine bado yupo tu hajaanza chekechea.
Nikawa nawapa vitu tofauti tofauti ila yule mama mjane akaniambia make sure unavyonipa vitu au kunisaidia mke wako asijue mana sisi wanawake tuna vitu vyetu rohoni siwez jua mkeo atachukuliaje hili suala la kunisaidia.
Basi tukaendelea kuishi hivyo mara paah nikapata kazi mkoani so natakiwa kuhama pale mtaani ila nikatulia kwanza sikuaga mpaka zimebaki siku mbili ndio nikaanza kupita kwa majiran kuanza kuaga wale tulio zoeana sana.
Nilipopita kwa huyu mama mjane kumuaga kama tunahama mkoa alisikitika sana sana sana. Siku ya pili aliniambia hivi unaondoka kweli au ulikuwa unatania? Nikamwambia ni kweli na tushamwambia dalali hapa tunapangisha dah alihuzunika sana akaniambia mimi jana sikulala huwez amini nafikiria unaondoka na ww ni mwenzangu sana unanisaidia na umekuwa kama ndugu sasa sio jirani tena.
Nikamwambia usijali bado tupo pamoja sana tutawasiliana kwa changamoto zozote zile. Basi tukaishia hapo ila funzo nililopata ni kuwa kwann yule alihuzunika sana? Mana nlichokuwa nampa hakikuwa kikubwa hivyo mimi sikuhisi kama ilikuwa kikubwa lakin yeye aliona ni kikubwa sana katika mtazamo wake hapa ndio tunapata Dhana ya kushukuru kwa kila kitu. Unachokiona ww kidogo kuna mwenzako huko anakiona kikubwa mno.
Alafu kingine nilicho kigundua ukitoa unapata zaidi ya ulichokitoa Amini hivyo.
Huyu mama akinipigia simu nina shida ya kitu fulani na nikamtimizia basi hiyo wiki au hiyo siku lazima ntapata zaidi ya nilichompa, kama kuna mtu atabisha kwa hili basi atakuwa ameamua tu.
Note: UKIMSAIDIA MTU UMEJISAIDIA MWENYEWE