Kama usafi wa vyoo umetushinda, kwanini tusivigeuze vivutio vya kitalii?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Tembelea vyoo vya uma vya hapa Tanzania ujionee maajabu! Vingi ni vichafu hakuna mfano.
~ vyoo vya vituo vya mabasi
~ vyoo vya sokoni
~ mpaka na vyoo vya baadhi ya mahospitali navyo vipo kwenye huo mkumbo.

Labda Watanzania wana utamaduni wa kuvipenda vyoo vichafu? Mbona sivyo ilivyo kwa baadhi ya majiji ya nchi jirani kama Kigali? Wao wana nini cha ziada?

Nimeviona vyoo vya uma vilivyopo kwenye bustani ya uma jijini Nakuru nchini Kenya! Kwa jinsi vilivyo visafi hutaacha kukubali kuwa wanaovisimamia wameshule wakashuleka!

Kwa kuwa hilo limeshindikana Tanzania, tuvigeuze viwe vivutio vya kitalii!

Tuwaalike watu kutoka Mataifa mbalimbali waje washuhudie mfano wa vyoo vichafu! Alau tufaidike kwa malipo watakayoyafanya.

Lakini kwa usalama wao, waje wakiwa wamevaa masks na wawe na sanitizers watakazoziaply kabla na baada ya kuvikagua hivyo vyoo

Bora tu tufanye hivyo ili ijulikane kuwa tumeamua kuvitumia vyoo vichafu kama vyanzo vya kipato.

Alau hiyo inaweza kutupunguzia aibu!
 
labda ni afrika nzima
nilienda choo hospital ipo kenya sehemu inaitwa bomet, mbele kidogo ya kisii ukitokea sirari ,ni kichafu sijawahi ona mfano wake

Kama ndivyo, basi pangestahili kuitwa "shithole countries", lakini siamini hivyo.

Sidhani kama hayo yapo Botswana na South Africa.
 
Kuna watu wamekariri kua Choo ni sehemu chafu kitu ambacho sio kweli kabisa,

Choo ndio sehemu ambayo inatakiwa iwe safi zaidi,

Hii ni issue ya mindset tu mkuu,watu wakibadili hii fixed mind mentality na kujua kua Choo ni sehemu inayotakiwa kua safi muda wote,basi hapo mabadiliko yatakuja tu,hii elimu itolewe kuanzia mashuleni kwa watoto wetu,pia wazazi nao waelimishe watoto wao kwenye issue ya usafi wa mazingira na kutokutupa uchafu hovyo,

Ni ngumu sana kumbadili mtu mzima,ndio maana nashauri elimu itolewe kwa watoto ili huko mbele kuwe na mabadiliko ya kiujumla katika suala la usafi,

Usafi ni tabia.
 
Hizo nchi kuna watu wanalipwa kwa kufanya usafi kila saa
Yaani uangalizi wa mda wako wa kazi wote
Wewe ni usafi wa Choo tu
Sasa sisi Choo mpaka msafishaji hakuna ila kuna vya kulipia vina unafuu
Ila watu wachafu aisee
Lakini pia wahusika wangekuwa wanapigwa faini washike adabu
 
Vyoo vyetu vya majumbani vp napo
Haha

Ova
 
Tembelea vyoo vya uma vya hapa Tanzania ujionee maajabu! Vingi ni vichafu hakuna mfano.
~ vyoo vya vituo vya mabasi
~ vyoo vya sokoni
~ mpaka na vyoo vya baadhi ya mahospitali navyo vipo kwenye huo mkumbo.

Labda Watanzania wana utamaduni wa kuvipenda vyoo vichafu? Mbona sivyo ilivyo kwa baadhi ya majiji ya nchi jirani kama Kigali? Wao wana nini cha ziada?

Nimeviona vyoo vya uma vilivyopo kwenye bustani ya uma jijini Nakuru nchini Kenya! Kwa jinsi vilivyo visafi hutaacha kukubali kuwa wanaovisimamia wameshule wakashuleka!

Kwa kuwa hilo limeshindikana Tanzania, tuvigeuze viwe vivutio vya kitalii!

Tuwaalike watu kutoka Mataifa mbalimbali waje washuhudie mfano wa vyoo vichafu! Alau tufaidike kwa malipo watakayoyafanya.

Lakini kwa usalama wao, waje wakiwa wamevaa masks na wawe na sanitizers watakazoziaply kabla na baada ya kuvikagua hivyo vyoo

Bora tu tufanye hivyo ili ijulikane kuwa tumeamua kuvitumia vyoo vichafu kama vyanzo vya kipato.

Alau hiyo inaweza kutupunguzia aibu!
Nikisemaga humu waafrika hata kunya tu ipasavyo hatuwezi ninabezwa
 
Hata vyoo vya magogoni na bungeni vichafu. Uchafu na waafrika:

4349153_zuma_jpeg2b1a6f4ae132cd6683adb4edad2d2518.jpg
 
Back
Top Bottom