Kama Wafu wasingesemwa, tusingekuwa na somo la Historia

Kama Wafu wasingesemwa, tusingekuwa na somo la Historia

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Nimeona watu wanatema mapovu mtandaoni kuwa ni vibaya kuwasema watu waliokufa, hata kama walifanya mabaya kiasi gani

Kama watu waliokufa hawasemwi, basi tusingekuwa na somo la historia

Historia ambalo ni somo muhimu zaidi kwenye siasa, msingi wake ni kuyasema mambo yaliyofanywa na wafu, mabaya au mazuri
 
Leo katika Histori 1 mwaka 2056 Katika topic ya Uthubutu kwa Nchi Tutaenda kujifunza Juu ya MTU mmoja anaitwa Kazi Ndu-Guy mnamo mwaka 2022 bwana Kazi Ngu-Guy awiwaambia umma kuwa "Hii nchi itakuja uzwa hii" na hiyo ndo ilikuwa kauli yake ya mwisho bwana kazi kusikika kwa hadhira
 
Tuache uongo, jiwe alikuwa dikiteta wa ajabu kuwahi kutokea.

Kuficha madhambi yake alienda kanisani kila jumapili na waandishi wa habari na wapiga picha za mnato na video.

Na ili kughilibi watu zaidi kila mara alikuwa anaomba tumuombee.
 
Alikuwa mojawapo ya watu waovu kuwahi kutokea duniani
 
Hitler, Pinochet, Musolin, Mobutu, Amin, Pol Pot, Bokasa. Hawa ni baadhi ya viongozi wanaosemwa kwa mabaya kila kukicha. Mobutu hata kifo chake hakikutangazwa. Haoa kwetu Amin alipokufa tuliona kama mzoga tu. Serikali wala haikujishughulisha kupeleka salamu za rambirambi.
Na viongozi hao wote walikuwa wanapendwa sana na watu maskini kwa maelezo kuwa wanawatetea.
Leo hii wanasemwa vibaya mno.
Walitenda mabaya kwa jina la wanyonge kusemwa vibaya.
 
Back
Top Bottom