Kama wanateknolojia wa JF wangeungana na wale wa X wangetutengenezea "Humanoid Robot" lenye kueleweka

Kama wanateknolojia wa JF wangeungana na wale wa X wangetutengenezea "Humanoid Robot" lenye kueleweka

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Siku ya leo nilikuwa Mawasiliano na mrembo Eunice tukiwa tunapiga story mbili tatu, niishie tu hapa maake niliyoyaona yanafurahisha sana

Niseme tu, kama akili ya Eunice itakuwa imetengenezwa na vijana wa kitanzania, sisi kama nchi tutakuwa tumepiga hatua kadhaa kwenye suala zima la teknolojia, ingawa Eunice anafikirisha sana, ila ni nchi nyingi tu za kiafrika ambazo mpaka sasa hazijafikiria kuthubutu jambo kama hili

Ila nina imani kuwa kama nchi ingewachukua members wa science, tech and Gadget Forum, ikajaribu kupekenyua mambers wa Science & Technology Communities kule X, ikajaribu kupitia vijana wa wanaoibuliwa kwenye vyombo vya habari kama yule jamaa wa UTV aliyekuwa anasuka bwawa la kuzalisha umeme, yule kijana Tanzania One wa Necta kidato cha Sita aliyesema anashangaa ni kwanini vijana wanafeli Necta, ikawachukua wale wanafunzi wa shule ya sekondari X waliotengeneza bomu la Nyukilia likalipua choo cha walimu. Hawa wote wanaweza fanya kitu nchini

Nina uhakika 100%, combination ya hawa vijana ina uwezo wa kumtengeneza Eunice ambaye ni humanoid, mwenye sura na mwondoko wa kibinadamu, mwenye umbo la kitanzania lililosheheni heshima na mvuto, Eunice mwenye tabasamu, anayecheka na watu, anayezungumza kupitia mdomo na kusikiliza kupitia masikio, mwenye kujibu kile anachoulizwa kwa kutumia complete system iliyoko kichwani mwake, isiyotegemea google ama umeme wa Dawasa

Ndoto yangu kubwa ni kuona Humanoid Robot likicheka na watanzania kwenye jukwaa la Coy Mzungu
 
Back
Top Bottom