Uchaguzi 2020 Kama wapiga kura wa tarehe 28, Oktoba 2020 wakilifuata tangazo la NEC redioni, kuna uwezekano kura zikapigwa kwa wiki mbili

Uchaguzi 2020 Kama wapiga kura wa tarehe 28, Oktoba 2020 wakilifuata tangazo la NEC redioni, kuna uwezekano kura zikapigwa kwa wiki mbili

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
NEC najua hapa JamiiForums mpo na 'mnanikodolea' zenu huku wengine hata mkiwa 'mnaninunia' pengine kwa 'Kuwasema' Kwangu ila nina bahati mbaya moja tu Mimi ni kama Bahari ambayo daima huwa haikai kamwe na Uchafu hivyo 'mnivumilie' tu na 'mnizoee' vile vile. Msiposemwa hamtobadilika na mkibadilika sasa mapema yote hii basi ndiyo Furaha yangu pamoja na Wapiga Kura wote waliopo.

Nimetoka 'Kulisikiliza' Tangazao lenu hasa lile la 'Redioni' linalohusu Upigaji Kura hapo tarehe 28, Oktoba 2020 na 'Maelekezo' yake yote. Kwa namna tu 'nilivyolisikia' na hata 'linavyosikika' Redioni kiukweli linakatisha mno 'Tamaa' Wapiga Kura kwani inaonyesha kuwa Siku hiyo ya Kupiga Kura Yule Mpiga Kura atakuwa na 'Mlolongo' mkubwa hadi akamilishe hilo 'Zoezi' la Kikatiba.

Nijuavyo Zoezi la Kupiga Kura linatakiwa liwe ni 'Rafiki' na lenye 'Mvuto' na 'Ushawishi' hasa wa 'Kimawasiliano' kwa Walengwa Wakuu ambao ni Mimi GENTAMYCINE na Watanzania wenzangu takribani Milioni 29 ambao tumejiandikisha. Tangazo lenu kama ukilisikiliza unaweza kudhani kuwa Kupiga Kura kutachukua ama Wiki Moja au hata Mbili.

RAI yangu Kwenu NEC na hasa kwa Mkuu wenu wa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Mawasiliano 'Mwanahabari' Dkt. Cosmas Mwaisobwa hebu lipitieni 'upya' na tumieni 'Mbinu' za 'Kimawasiliano' ili likienda 'hewani' liweze Kumfanya Mpiga Kura awe na hamu ya Kwenda Kupiga Kura Siku hiyo na lisimfanye Mpiga Kura aanze Kukata 'Tamaa' mapema kwa 'Kuhisi' kuwa atachelewa au ataboreka na Zoezi hilo zima.
 
Mturudishie kodi zetu kwanza hata mimi sintopita hapo, kodi zetu mrudishe, na tutakaopigia kura upinzani mtuondowe kwenye orodha ya walipa kodi

Pia msisahau kama mtaiba kura na kupata Rais huyu huyu mbaguzi basi majimbo yote yatakayookuwa ya upinzani ukianzia Kigoma, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Iringa, Dar, Mara and likes majimbo hayo yote mziondoqe ofisi za TRA mzihamishie Kongwa na Mtera kwa misukule yenu.
 
Kura haziwezi kupigwa zaidi ya siku moja, tena mwisho ni saa kumi na mbili jioni, gao NEC wasitake kuleta mchezo wowote wa kitoto utakao hatarisha amani.

Kura siku mbili tangu lini?!!
 
Hilo tangazo mnasemaje maana sisikilizi radio TBC. Mimi nakuja radio za music kwenye gari na CD zangu na usb
 
Kura haziwezi kupigwa zaidi ya siku moja, tena mwisho ni saa kumi na mbili jioni, gao NEC wasitake kuleta mchezo wowote wa kitoto utakao hatarisha amani.

Kura siku mbili tangu lini?!!

Mwaka huu UCHAGUZI ni siku mbili(2)

1. Maaskari na Watumishi wa Tume,

idadi yenu inajulikana,

ole wenu mchague UPINZANI mtajuta.

2. Raia, idadi yenu inakadiriwa kuwa ni zaidi ya MILIONI 28 (ishirini na nane)

kutokana na makadirio hayo, Tume ya Uchaguzi itapanga MATOKEO kwa jinsi itakavyoona inafaa.

MAAMUZI YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI HAYAHOJIWI POPOTE PALE.
 
Tume walitarajia uchaguzi wa tarehe 28 utakuwa kama ule uchaguzi wa serikali za mitaa ili wafanye udhalimu na dhuluma ila wanaona hesabu na mbinu zao zinaelekea kugoma.
 
Bahati nzuri watumishi watakaosimamia uchaguzi Ni ndugu zetu tunaoishi nao pamoja.
 
Mambo ni fire hata Wachaga wamekuwa Wakurya tena zidi mpaka na itochi usiki bila kuogopa chuo cha Polisi kuwa jirani Ccm jitafakarini mnakumbuka 2015 mlikuwa mnaficha sare zenu?
 
Back
Top Bottom