Kama wataka ijua meetnawe na ulikosa mahojiano yetu na radio free africa(rfa) jana, ijue/uliza hapa

meetnawe

Member
Joined
Aug 1, 2013
Posts
9
Reaction score
1
Tunashukuru sana kwa watanzania wote wanaoendelea kutuunga mkono na kuikuza meetnawe, shukrani pia ziende kwa Radio Free Afrika - Mwanza, Tanzania kwa kuona thamani yetu na kutuunga mkono katika vipindi vyake vya wiki iliyopita na jana usiku.

MEETNAWE ni mtandao mpya wa kijamii uliotengenezwa na vijana wa kitanzania ulioanza kutumika taklibani miezi 3 iliyopita. Humu tumechanganya features za fb,twitter na kuongezea nyinginezo kama vile kuna PUBLIC CHAT: hapa watu wa nchi moja au na nyingene wanapata fulsa ya kuchat kwa pamoja na hata wanafunzi kuweza kufanya group discussions. Pia kuna akaunti maarumu kwa vipindi vya Radio na Televisheni, akaunti hii ikiwa na topics and news, polling area, request zone, suggestions box e.t.c... Kwa hili ina mana mtumiaji ataweza kuskiza au kuangalia kipindi akipendacho huku akiendelea kuwasiliana na wenzake, na mengineyo mengi.

Kwa kuijua zaidi tafadhali tembelea Welcome Welcome na tunakaribisha maswali pia hapa.
 
Nilifungua a/c yangu ya meetnawe lakini sijaenjoy hata kidogo...

Kwanza imepooza kama blog za MICHUZI..
 
Hii ni kwa ajiri ya vipindi vya radio na televisheni
 
Ni Bure kwa akounti zote, za kawaida na za radio/televisheni
 
Ha ha ha, ila kama mfumo na namna inavyotumika umeielewa basi hili wala usitie hofu... Hata mbuyu nao ulianza kama mchicha unakumbuka? 90% ya sites mpya zinazoanza huanza hivyo. Ntahakikisha hautakua bored tena. Ila asante kwa sapoti

Nilifungua a/c yangu ya meetnawe lakini sijaenjoy hata kidogo...

Kwanza imepooza kama blog za MICHUZI..
 
Nimefungua tu nakutana na hii..!

Write Upload Refresh

No friends posts
Contacts: 0
Following: 0
Followers: 0
Sign out as Window7
Back to top
Notifications (0).

Sasa hakuna ku edit data zangu? Kwa nini kabla sijawa member kamili nisijaze info zangu kuliko hii short cut mliyoiweka?!

Nimeipenda hii kwakweli coz si ya nyumbani.!

Ila jinsi yakusajili members ndio inabooooa.!!!!
 
Nipe jinsi ya kujiunga naandikaje website yenu?

kuna form ya sign up utajiza jina, email na password tu, then tutakutumia email ili kuhakiki.
Kama watumia simu bonya sihemu iliyoandikwa sign up itakupeleka kwenye fomu ya kujiunga
 

Asante sana kwa taarifa hii, ni kweli ilitakiwa ikupeleke kwenye page ya ku edit taarifa zako, nafikiri baada ya dk30 itakua hivyo. Na asante saaana kwa kuipenda
 
nimeingia ila nimeshindwa kitu kimoja kwaamba nimpaka utengeneze marafiki ndipo unapoweza kusoma habari kwenye tahrir sasa kama sijawafaham watu nawezaje kutengeneza hao marafiki??

na kwann msiache watu waweke habari zao kisha wengine wachangie kama tulivyozoea??
 
Katika tahrir tukifanya kila mtu akaandika habari bila hata ya kua na rakifi, hii inaweza ikatumiwa na watu vibaya, yani mtu anaweza akajiunga tu ili kwenda kuweka ujinga au matusi, sasa ili kuzuia hio ndio mana tumefanya ili kupost basi tunataka tuwe na ukakika kwamba kuna jamii inakujua kwa kukufollow. Asante kwa ushauri, nahisi itabidi tupunguze idadi ya rafiki wanaohitajika kukufollow ili upost katika tahrir, shukrani kwako. Kutengeneza rafiki watakiwa kwenda kweye link iliyoandikwa friends kama watumia kompyuta au tablet, na kwenye picha ya kichwa cha mtu chenye alama ya kujumlisha kama watumia simu.

 
Big up brothers, nakumbuka nishawahi kuandika kuhusu site yenu. Kazeni buti mtufurahise
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…