Kama Watumishi wa Umma wangekuwa wanakopeshwa nyumba na magari baada ya kuajiriwa

Kama Watumishi wa Umma wangekuwa wanakopeshwa nyumba na magari baada ya kuajiriwa

BABA SANIAH

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2013
Posts
4,606
Reaction score
5,922
Salaam Wana jukwaaa,

Nataraji mko bukheri wa afya, kwa wale wenye afya yenye mushkeli Bai nawombea Kwa MOLA, awafanyie wepesi wapate kupona na kuendelea na majukumu Yao ya hali, ila kama ya haramu hapana. Katika utumishi wa umma inaonekana Kuna ufisadi sana wa Mali za umma ha fedha.

Hivi kwa mfano baada ya watumishi wa umma kuajiriwa wangekua wanakopeshwa magari ya kawaida tu au Yale yasiozidi milioni ishirini,na kukopeshwa pia nyumba za kawaida vymba vitat au vinne, wakawa wanalipa kidogo kidogo.

Hivi Kuna mtumishi wa umma angefanya ufisadi au wizi kweli? Maana watu wanaiba Ili kujenga majumba na kununua magari, Sasa vyote umeshapata hivi utaiba Ili iwe Nini?

Nadhani ni fursa Kwa wafanyabiashara kufanya hiyo kitu Ili kupitia serikali kufanya hiyo kitu,kama yalivyo mabenki,yanayokopesha watumishi mkopi mpaka wa miaka minane Kwa watumishi.

Binafsi sioni tatizo kama mtumishi ana contract ya permanent and pensionable terms akikopeshwa mkopi hata wa miaka ishirini ukiwa atapewa vitu kama nyumba na gari.

AHSANTE KWA KUSOMA BANDIKO LANGU[emoji120][emoji120]
 
Wizi ni tabia,
Mwizi huongozwa na tamaa
Na tamaa ikishawaka Haina kikomo
Asilimia kubwa ya mafisadi sio maskini
 
Wezi wana madaraja yafuatayo:-

- mdokozi
-kibaka
-jizi
-jambazi
-fisadi
-bepari
-beberu

Hizo ranks zote wanatofautiana ni mzgo Kias gani wanaiba.

Kuanzia level ya jambazi,kushuka chini
Hawa Ni wezi professional wenye mitaji, kamati na wamejipanga hawakurupuki.

Wezi Hawa hawaibi kusurvive Bali kujiongezea na kujilimbikizia ukwasi[emoji4]
 
Wezi wana madaraja yafuatayo:-

- mdokozi
-kibaka
-jizi
-jambazi
-fisadi
-bepari
-beberu

Hizo ranks zote wanatofautiana ni mzgo Kias gani wanaiba.

Kuanzia level ya jambazi,Hawa Ni wezi wenye mitaji, hawaibi kusurvive Bali kujiongezea na kujilimbikizia ukwasi[emoji4]
Lakini wanaoongoza kuuliwa ni kibaka jizi na jambazi mara chache kwa mwaka, kwanzia mafisadi hawaguswi kabisa
 
Lakini wanaoongoza kuuliwa ni kibaka jizi na jambazi mara chache kwa mwaka, kwanzia mafisadi hawaguswi kabisa
Mafisadi Ni wezi professional wenye system na connection Kali Sana.

Wanaiba pesa ya maana Kias kwamba inatosha kabisa kuajiri mawakili ,kuhonga waendesha mashtaka na majaji wote wakafunga domo lao kimya na kubakiwa na chenji kadhaa za kufanyia fujo mjini.
 
Back
Top Bottom