mi kijana wa kiume,umri wangu ni miaka 28,nipo dar.
hapa naona tatizo..wewe ni kijana wa kiume...kijana wa kiume ni tofauti na mwanaume.. Tafakari na chukua hatua....umri wa miaka 28 tutajuaje
nahitaji mwanamke wa kuoa mwenye sifa zifuatazo
unahitaji..means mke ni mahitaji kama bidhaa za nyanya, vitunguu etc... Hebu tafakari vizuri
-awe mcha mungu,kristo
kwa hiyo mnataka mkioana mufungue kanisa kama kakobe?
-umri kati ya miaka 20-25
umri ni namba tuu...afterall wee nae bado mtoto unataka kuoa mtoto wa 20 -25 yrs ambao woote wako shule na vyuoni wanasoma
-awe mwenyeji wa mikoa ya kanda ya ziwa au mkoa mwingine wowote isipokuwa arusha na kilimanjaro
ubaguzi wenye asili ya ukabila...hutofika mbali kwa tabia hii
-asiwe mnene sana ila kama mwembamba mrefu ni sawa lkn sio lazima
means hutahitaji kununua ngazi hapo nyumbani kwenu?
-elimu isiyopungua kidato cha 6 na isiyozidi degree 1
elimu ya nini?...means mnataka kuanzisha shule hapo nyumbani kwenu au unahitaji mwenye elimu hii ambayo wenzako wanalalamika kila siku kuhusu wanawake wasomi..kwanini usitafute mwenye cheti cha elimu ya ndoa na mahusiano ya jamii
-asiwe na mtoto wala hajawahi kuolewa
means ukishamuoa huhitaji azaee?...au ndio baadae unaanza kulalamika mkewangu ashiki mimba?...nadhani la kuwahi kuolewa ni suala la experience..soo kigezo cha experience in marriage huiitaji?..soo unahitaji awe bi-kira?
mambo mengine ni ya kuongea sisi wawili
mambo gani zaidi ya haya uliyoweka hapa?..mbona naona ushaongea yote au ni umbea unataka kuonge na muhusika privately?
Kama unamaanisha na una sifa hizo naomba tuwasiliane,na nikimpata nitatoa taarifa kwa wana jf ili kusiwepo na usiri na ijulikane kuwa nina mtu tayari
kwani wewe mwenyewe unamaanisha?..onyesha jinsi unavyomaanisha sio kuja na kuandika hapa kirahisi namna hii
nawasilisha