BABA TUPAC
JF-Expert Member
- Sep 30, 2015
- 1,527
- 3,811
Wanabodi,
Clouds Fm wanafanya show yao ya Fiesta tarehe 25 Nov huku EFM pia wakifanya show yao tarehe hiyo jijini Dar tena bure, Dar ina watu wengi lakini ni kweli usiopingika kuwa lazima kuna mmoja ataathirika kibiashara. Ili ni jukwaa la biashara nadhani tungekuwa tunajadili mambo halisi kama haya yangesaidia kutujenga kibiashara, je kama wewe ni mmiliki wa mmoja ya vituo vya radio ungefanya nini?
A. Ningekuwa mmliki wa Clouds fm au nipo katika management ningefanya yafuatayo;
1. Ningechukua wasanii wote wanaovuma kwa wakati huu - hii ingewakosesha wasanii bora hivyo watu wengi watakuja kwenye fiesta
2. Kwakuwa Clouds ina ushawishi kwa wasanii wengi na wengi wanaiogopa kwakuwa inaaminika ukigombana na Clouds basi huwezi kukua kimuziki, basi ningepandikiza propaganda ya chini kwa chini kuwa msanii yeyote atakayeenda kufanya show ya EFM hatutapiga tena nyimbo zake wala kumuita kwenye show - hii itasaidia kupunguza wasanii wazuri kwenda EFM hivyo watapata watu wachache
3. Mara nyingi show za Dar huwa ni bei kubwa, basi ningeweka punguzo ili kukabiliana na ushindani uliopo mbele yangu
4. La mwisho, katika matangazo yangu ya show ningeongeza nguvu zaidi kuwasisitiza watu wanapoenda kwenye show wazingatie usalama wao ''vya bure gharama''
B. Ningekuwa mmliki wa EFM ningefanya yafuatayo;
1. Kwakuwa Diamond ana mkataba na Vodacoma hivyo moja kwa moja hawezi kufanya ''Tigo Fiesta'', kwahyo ningemchukua kufanya show yangu - ningepata mashabiki wengi ambao hawamtaki Alikiba, kumbuka Alikiba atakuwepo Fiesta
2. Kwakuwa show yangu ni ya bure, hivyo ningewekeza nguvu kubwa sana kufanya matangazo yangu kwa wakazi wa maeneo ya Tandale, Manzese, Mbagala, Buguruni na maeneo mengine ambayo inaaminika kuwa wanaishi zaidi watu wa hali ya chini. Hii ningetumia magari na bodaboda - hii itanisaidia kuongeza zaidi aina ya watu watakaohudhuria
3. Kwakuwa vijana wengi wameathiriwa na bahati nasibu/betting, ningeingia ubia na kampuni ya Biko au Tatu Mzuka na kuahidi kuwa siku hiyo ya show atatangazwa mshindi wa milioni 80 - hii itasaidia kufanya vijana wengi zaidi kuhudhuria show hii ili kusubiri kuona mshindi ni nani? huenda akawa yeye
Je, ungekuwa wewe ungefanya nini ili kupata mashabiki wengi? chagua kampuni moja kisha weka mikakati yako