4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 8,406
- 9,619
Wakuu salama? Niwasalimu kila mmoja kwa imani yake popote mlipo wana - JF.
Mada hii fupi sana: Kama wewe ni sehemu ya watekaji tubu na jiandae, Mungu amenionesha pigo kubwa juu yenu.
Akinionesha mfano wa mmoja wenu ambaye ni mtekaji, alifika mahali tulipokuwa ambapo ilionekana kuna watu wengi kama vile kulikuwa na matukio mawili:
Ndani ya mshangao, alitokea kijana ambaye binafsi nilimwona kama sura ya rafiki yangu niliyesoma naye, ingawa hatuna mawasiliano kwa muda. Alionekana amechoka sana, akitembea kwa shida na nguo zake zimechakaa. Aliletwa na gari ndogo akiwa ameambatana na baba mmoja na mama mmoja kama wasamaria wema, lakini moyoni nikaambiwa kuwa alitekwa. Yule kijana akaambiwa apite nyuma ya nyumba na watu waliokuwepo pale, na yule mzee akatoa elfu kumi za Kitanzania kama msaada kwa kijana huyo.
Pale tulipokuwa tumekaa, mtu mmoja alipigiwa simu kutoka kwa mtu aliyekuja na gari kupitia barabara ya Magharibi, akamchukua mtu mmoja kwa haraka kuelekea kwenye gari la aliyepiga simu, na gari hiyo ikaondoka haraka.
Dakika moja baadaye, gari nyingine iliingia kwa kasi kubwa kutoka barabara ya Kusini, ambapo pembeni yake kuna gema, na ndani yake walikuwepo watu wawili: kijana wa makamo na mwili kidogo. Gari ilikata kona mbele yetu, lakini ilipotaka kurudi nyuma, ikatumbukia kwenye gema.
Gari hiyo ilikuwa na yule kijana mmoja na dereva wa pili, ambao wote walivunjika miguu huku wakitokwa na damu na wakiomba msaada. Watu walipojitokeza kuwasaidia, mmoja alisema kuwa wale ni watekaji, na kichapo kikaanza. Wengine walipendekeza wakatwe mikono. Mmoja alijitambulisha kuwa anatoka Kigoma.
Soma Pia:
Kumbuka: Siku zote watenda madhambi huwa watu wa kudharau. Kama wewe ni mtekaji, ukitaka kubali sawa, hutaki pia sawa, lakini kiama chenu kinakuja. Sijataka kwenda kwa undani sana, lakini nimeonyeshwa mengi. Anzeni kuandaa makaburi yenu.

- Maandalizi ya mtu mmoja kufunga ndoa.
- Mama aliyejifungua akitafutiwa ndizi kwenye shamba fulani.

- Wananchi na Viongozi wa Upinzani kukaa kimya kunatoa mwanya kwa watekaji kuendelea kupoteza watu nchini
- TLS kuandaa kongamano la Kitaifa kuhusu matukio ya kutekwa na kupotea kwa raia nchini Tanzania