Kama Wewe Unauelewa Wa Tv's Na Brands Zake Pita Hapa

Mr Justin

New Member
Joined
Sep 14, 2019
Posts
2
Reaction score
0
Habari za wakati huu wakuu?? Natumaini wote ni wazima wa afya na mnaendelea vizuri na majukumu ya kila siku

Moja kwa moja niende kwenye lengo la uzi huu mimi nataka nifungue biashara yangu( )ambayo itanihitaji ninunue tv ili kuifanikisha kama moja ya mahitaji ya biashara husika tv ninazo zihitaji ni kwanzia nch 43+ nimeangalia brands kubwa kubwa kama Lg,Samsung,Toshiba,Tcl,Hitach na nyinginezo ambapo bei zake zinaanzia 800k (sio smart)

Lakini brands hizo hizo nimefuatilia second hand zinaanzia kwenye 650k ambazo zina ukubwa huo huo mean 43+ na bado zipo kwenye condition nzuri

Upande wa pili nimeangalia brands za kawaida zenye bei rafiki kama Star x,Abooder na evvol na nyinginezo zenye ukubwa wa inch 43+ ambazo ni mpya bei zake zinaanzia 650k na kuendelea

Tuje upande wa quality kutokana na uelewa wangu na nilipo zifanyia comparison naona hazitofautiani sana hata kwenye kudumu nimesikia zinadumu kulingana na utunzaji wako

Sasa kwa wajuzi wa haya mambo naombeni ushauri wenu kwa budget yangu ya 700k nichukue hizo brands za kawaida mpya au nichukue brands kubwa ambazo ni used kwakuzingatia vigezo vya ubora wa picha,bei na namna zinavyo dumu
 
...miyeyisho yake ipo wapi km zote ni HD na smart vilevile mkuu chukua hata izo nyingine sababu zote zina features sawa tofauti ni brand tu
 
Mimi kama fundi nakushauri kwa bajet hiyo chukua tv mpya hata ya kichina zinadumu sana tena kuliko hao samsung ila chukua inayo sapoti na upande wa DC
Ukutumia adapter kwenye tundu la dc inadumu zaid
Mtumba utarudi nyuma ya tecnology...
Hapo ni sawa na kuacha tecno phanton 9 mpya ukanunue HTC ya mwaka 2014 jelly bean storage mb 512
 
vipi kama hiyo used features zake ni zakisasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…