Kama Yanga haikualikwa basi ni kweli TFF ina chuki/mgogoro dhidi ya Yanga

Ameweka kituko aliposema jengo la yanga lilitumika kufanya vikao vya Siri kuwapumbaza wakoloni wakati jengo lao limejengwa Kwa msaada wa karume baada ya nchi kupata uhuru
Hii klabu imejaza Mashabiki vilaza watupu. Nahisi ubongo umeshachanganyikana na kinyesi.
Mtu anazamisha apewe heshima badala ya kutambua kwamba heshima inajileta yenyewe kama kipara .

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Nafikiri shida ni kiwa yanga wanaiwazia sana simba.

Simba isingeshiriki huo mkutano basi hata yanga wasingelalama.
shida ni wao kutaka kujilinganisha na simba.
Hata ile chenga ya mdhamini mkuu wa club niliifurahia sana. Ifike muda kila mtu avune alichopanda.
 
Naliona anguko la TFF ndani ya muda mfupi ujao. Kwa style inavyoongoza mpira nchini itaendelea kufanya kazi ya kujieleza siku hadi siku.
Unaonaje mkijiita CAF halafu mkaitisha mkutano wenu halafu mkaacha kuwaalika TFF ili nanyi muwakomowe?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 

Wahuni kwenu ni vijiweni tu mkigongeana vipisi vya bangi. Jifunzeni adabu na ustaarabu kwanza
 

Attachments

  • JamiiForums-157563313.jpeg
    45 KB · Views: 3
Ulivyoanza nikajua huko utopoloni kuna mtu wa tatu amekuwa discovered kumbe big NO. Pale uto Waheshimiwe sana wazee wawili hawa JK na SM
 
Huo mkutano ulitangazwa sana na vyombo vya habari muda tu kuwa utafanyika Arusha. Na mikutano yote mikubwa huwa na taratibu zake hususani wanaotakiwa kuwa washiriki wa mkutano na wajumbe waalikwa na wakati mwingine hata washiriki/wasikilizaji binafsi nao hupewa taratibu za kushiriki. Iwapo viongozi wa Yanga wangekuwa makini wangeshaingia kwenye tovuti ya CAF au hata kupiga simu huko CAF kujua taratibu zipoje na wao wakitaka kushiriki wafuate taratibu zipi. Na kama wasingepata ufafanuzi mzuri basi wangewasha magari yao toka Salamander mpaka ofisi za TFF Karume kuongea na viongozi wa TFF juu kushiriki kwenye mkutano Arusha jambo ambalo naamini kabisa wangepata maelekezo ya kutosha na huenda wangekuwa washiriki.

Kwa viongozi wa Yanga kuja kulalamika kwenye vyombo vya habari na kuilalamikia TFF tena baada ya mkutano wa CAF kwisha sidhani kama ni sahihi sana. Na pia wakati mwingine wakubali kujifunza kwa viongozi wenzao wa Simba kwani sio dhambi hasa ukizingatia mambo ya kushiriki kwenye mikutano na makongamano ya kimataifa haiathiri kabisa matokeo ya uwanjani kati ya Simba na Yanga. Babra mara nyingi tu anaonekana mitandaoni yupo CAF Cairo na juzi juzi tu hapa alikuwa Ghana kwenye mkutano mkubwa yote hiyo inamweka Babra na Simba kwa ujumla wake kwenye "platform" soka za Afrika na Dunia kwa ujumla wake.

Kwa upande wangu angekuwa amelalamika kiongozi wa zamani mzee Msola nisingeona tatizo kwani yeye ni kizazi cha "analogue" lakini malalamiko yanapotolewa na Hersi + Arafat hawa hawa wa "dot.com" napata shida kweli kweli kuwaelewa. Maana hawa wanasafiri sana nje ya nchi, wanawasiliaana na mawakala wachezaji na wachezaji wenyewe kila siku. Vipi walishindwa kuwasiliana CAF moja kwa moja kama wanaona viongozi wa TFF hawajawaalika kushiriki?

Ni matumaini yangu kuwa Hersi na Arafat watalichukulia hili suala la mkutano wa CAF uliofanyika Arusha kuwa changamoto chanya na kuwa wamejifunza kitu cha ziada kwenye uongozi wao. Bado wana mengi ya kujifunza na mengi ya kufanya vizuri kiasi cha kuthibitsha kuwa viongozi vijana wakiaminiwa kwenye soka wanaweza kufanya makubwa ya kupigiwa mfano.

Ni mtizamo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…