Kama Yanga wanadai bado kuwa Morrison ni mchezaji wao,ni nini hatma yake?

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Nimemsikia mwenyekiti wa Yanga akidai kwamba mkataba ulikuwa na mapungufu na mapungufu siyo sababu ya kuvunja mkataba.

Naomba kujua kisheria,je ni mapungufu yapi yanaweza kuchukuliwa ni ya kawaida na hivyo hata kama upande mmojawapo kati ya walioingia mkataba akawa hakuridhika analazimika tu kuutekeleza ukiwa na mapungufu hivyo hivyo?

Je TFF walikosea kuwabeba Yanga kwa kulibadili kosa la ku temper na mkataba kuwa mapungufu ya kimkataba tu?

Vipi nalala aliyokuwa nayo Morrison, imefanyiwa mabadiliko hayo yaliyoonekana mapungufu tu?

Kwa nini Yanga hawakuadhibiwa kwa kujaribu kudanganya kuhusu mkataba wa Morrison?

Ni kweli viongozi wa Yanga hawana wanasheria wa kuwaelewesha kuhusu masuala ya makosa ya kujaribu kughushi?

Vipi ile saini iliyosemekana si ya Morrison, vyombo vya ulinzi waligundua nini?

Nahisi sakata hili linaweza kuja na mengi kuonesha udhaifu mkubwa wa viongozi wa mpira nchini.
 
We subiri fimbo ya fifa inakuja
 
Yanga kwa BM awanachao.viongozi wa Yanga acha tu waendelee kuwazuga mashabiki wao ili wazibe mapungufu yao.
 
Kwa mana hiyo viongozi wa yanga ni utopolo wa kiwango cha mwisho maana haingi akilini eti clab kubwa kma yangu kufanya mkatába wa kijinga namna ile ni upuzi mtupu
 
Tff wenyewe ndio walio mwidhinisha Morison yanga, Afisa usajili wa Tff anaye shughulika na TMS kwaniaba ya shilikisho ilo Alisha fanya iyo kazi tangu mwezi wa tatu mwaka 2020.
Hivi namba ya kuchangia tununue wachezaji wawili imetoka, nataka niwachangie watani zangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…