Kamala Harris ampigia simu Rais Trump kumpongeza na kukubali matokeo ya uchaguzi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Makamu wa Rais wa Marekani ambaye alikuwa Mgombea Urais wa Marekani 2024 aliyeshindwa dhidi ya Rais Mteule Donald Trump, amempigia simu Trump na kumpongeza kwa ushindi kitendo kinachoashiria amekubaliana na matokeo hayo ya uchaguzi.

Pia, Soma:

β€’ Yanayojiri katika Uchaguzi Mkuu Marekani 2024: Nani kuibuka kidedea?
β€’ Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Kamala amempigia Trump kumpongeza na wameongea pia kuhusu mchakato wa kukabidhi madaraka kwa amani na umuhimu wa Trump kuwa Rais wa Wamarekani wote bila kujali tofauti ya Vyama au Itikadi.
Your browser is not able to display this video.

Kambi ya kampeni ya Trump imepongeza alichokifanya Kamala wakisema ni ukomavu wa kisiasa.

Kamala ametoa hotuba ya kukubali kushindwa na mstakabali wa Serikali katika Chuo Kikuu cha Howard.
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Kamala Ameonyesha kukomaa kisiasa na uelewa wa demokrasia.

Moja ya misingi mikuu ya demokrasia ni pamoja na kukubali kushindwa na kuwa tayari kukabidhi madaraka kwa kiongozi mpya aliechaguliwa kihalali na wapiga kura wanojitambua.
 
Pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwezesha uchaguzi huo
 
Marekani ni mfano wa kuigwa.
Katiba mpya ndo soln kwa nchi nyingi za kiafrica
 
Nafkiri Samia akishindwa atampigia simu mbowe ama Tundu lissu kumpongeza, huyu ni mwanamke mwenzake amekubali matokeo bila ya hila zozote, anaumia lakini amejikaza huwezi ona tofauti
 
"And we will engage in Peaceful transfer of Power..." KAMALA HARRIS
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ«‘
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…