Kamanda Muliro: Maandamano yakifanyika hayajifichi, huwezi kuwa mtu mmoja unatembea ukasema nimefanya maandamano

Kamanda Muliro: Maandamano yakifanyika hayajifichi, huwezi kuwa mtu mmoja unatembea ukasema nimefanya maandamano

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
1687240833380.png

Maandamano yakifanyika hayajifichi, huwezi kuwa mtu mmoja unatembea ukasema nimefanya maandamano, nadhani hata kwenye kamusi ukitafuta neno maandamano unaweza ukaelewa maana yake ni nini, usalama uliimarishwa kiwango ambacho kiliruhusu watu kufanya shughuli zao.

"Tulimjibu mhusika na tukampa pia ushauri kuwa kama ana hoja au jambo la msingi ambalo ni sehemu ya haki yake bado zipo mamlaka za kisheria ambazo angeweza kufikisha hoja zake bila kuathiri haki za msingi za kikatiba za watu wengine"

"Dar es salaam ni mji wa kibiashara, miongoni mwa mitaji muhimu katika biashara ni usalama, kwahiyo jeshi likibaini aina yoyote ya matishio ya kiusalama jukumu kubwa ni kuzuia ili kusiwe na taharuki"

"Wakazi wa Jiji la Dar es salaam ni watu ambao hawataki matukio ya kihalifu na hawakubaliani na vitendo vya kihalifu" Muliro Jumanne Muliro , Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Canzo: EATv
 
Kwani mtu mmoja amezuiwa na sheria gani kuandamana akitaka?

Hawa polisi wa mkoloni wa Tanganyika wana matatizo sana.
 
Back
Top Bottom