Kamanda Muliro: Ndio maana sitaki kubishana, Jeshi la Polisi ndio lilimuokoa Sativa kule Katavi!

Hao wanaomuuliza hapo siyo raia kabisa. Hao ni polisi na ndiyo waiomuokoa.

Msidanganye watu.
Kwa hiyo hao wauliza maswali ni polisi na badala ya kumuwahisha kwenye matibabu wao ni interview tu? Bado sijaamini kwamba ndipo uwezo wetu wa kufikiri ndipo ulipogota…bado sana.
 
Kwa hiyo hao wauliza maswali ni polisi na badala ya kumuwahisha kwenye matibabu wao ni interview tu? Bado sijaamini kwamba ndipo uwezo wetu wa kufikiri ndipo ulipogota…bado sana.
Wasikilize vizuri, wameongelea hilo la hospitali.
 
Kwani we umejuaje kuwa hao siyo maafande,msipende kubishabisha vitu msivyovijua
Kiongozi, kuhusu chadema utafanya busara kubwa ukikaa kimya tu. Ni watu wa hovyo sana.......mapinga Pinga tu muda wote.
 
Kwani we umejuaje kuwa hao siyo maafande,msipende kubishabisha vitu msivyovijua
Hamna wajinga wa hivyo siku hizi boss. We kaa kimya tu maana mna mbinu so outdated wakati kizazi kimebadilika.
 
Hata kusingekuwa na hiyo video bado alikuwa hana ushahidi wa kutosha.

Kamuokoa dhidi ya akina nani? Mazingira ya uokoaji yalikuwaje? Walifanikiwa kuwakamata watekaji? Kama sio waliweza kuwatoroka polisi hadi leo bado hajawapata?

Huyu mzee akistaafu na kutazama baadhi ya kauli zake atasononeka sana.
 
Your browser is not able to display this video.
Akizungumza katika Kongamano la kujadili suala la utekwaji na upoteaji wa raia nchini Tanzania, Oktoba 5, 2024, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi lilishiriki katika kumuiokoa Edger Mwakalebela maarufu katika Mitandao ya Kijamii kama Sativa katika tukio lake alilotekwa na kujeruhiwa.

MULIRO: SI KILA JAMBO LIUNDIWE TUME, WATU WANA HAKI YA KUONGEA
DAR: Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ameitaka Jamii kuwa na kawaida ya kuheshimu mifumo ya Kisheria na Vyombo vinavyoendesha mifumo hiyo na kuwa sio kila jambo liundiwe Tume kama ilivyokuwa wakati wa Serikali ‘fulani’.

MULIRO: SI KILA ANAYEPOTEA AU KUTEKWA NI MWANA-CHADEMA
DAR: Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kesi zinazohusu utekaji zipo na zimeripotiwa katika jeshi hilo lakini si kweli kuwa wanaokutwa na changamoto hiyo wote ni Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Amesema hayo katika Kongamano la kujadili suala la utekwaji na upoteaji wa raia nchini Tanzania, Oktoba 5, 2024 kwenye jengo la Ubungo Plaza lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria (TLS)

Pia soma ~ TLS - Kongamano la kitaifa kujadili matukio ya utekwaji na upoteaji wa raia nchini Tanzania
 
Tunamezwa na taarifa za kina SATIVA nchi inaporwa kinyama,tumekuwa watu wa matukio kila uchao, pathetic
Kwani hatuwezi kuongea hayo ya Sativa na ya nchi kuporwa kwa wakati mmoja?

Kwani la watu kutekwa na kuuawa nalo si nchi kuporwa?

Kwani hapa JF huwa tunasema leo tuchangie uzi mmoja tu?

Kwani Watanzania hawawezi kujadili mada zaidi ya moja kwa wakati mmoja?

Why are you making this false dichotomy while all these things are about failure of keadership in oarticular and our sociwty in general?
 
Kuna vitu vinatia hasira Nchi hii Hadi unatamani upate mabomu uende kituo Cha polis ukajitoe mhanga kama walivyokuwa wanafanya waarabu. Mtu alitaka kuuliwa waziwazi na polisi halafu wanakataa Kwa nguvu zote.
 
Tunamezwa na taarifa za kina SATIVA nchi inaporwa kinyama,tumekuwa watu wa matukio kila uchao, pathetic
Kati ya kuporwa na watu kutekwa na kuuwawa kipi cha kwanza kupiga vita??
 
Tunamezwa na taarifa za kina SATIVA nchi inaporwa kinyama,tumekuwa watu wa matukio kila uchao, pathetic
Uporaji wa rasilimali upo kwa carne kuanzia waarabu, wazungu, na sasa waliopo. Ila haki ya kuishi pia lazima ipiganiwe, itetewe na kulindwa.
 
Kuna Watu wana mapepo ya Uongo.
 
Tunamezwa na taarifa za kina SATIVA nchi inaporwa kinyama,tumekuwa watu wa matukio kila uchao, pathetic
Kuna kitu cha muhimu kushinda uhai wa mtu?

Kwa hiyo tuache watu watekwe na kuuawa halafu kuzingatie kuporwa?
 
Mda mwingne kujitetea sana unaharibu n bora ubaki kmy tu! Dunia ilipofika mambo yapo wazi hakuna cha kufichana hayo n maisha kabla ya technology haijafika nchini
 
SATIFA aliokolewa kwa kuokotwa na rafiki yangu dereva wa gari la pikapu toyota aliyekuwa anatoka mpanda kwenda mpimbwe.dereva huyo alisimamisha gari na kushangaa kumuona mtu katika maeneo hayo na akiwa anavuja damu anatambaa kuelekea barabarani.rafiki yangu huyo anasema kuna basi liliwakuta pale nao wakaanza kumshangaa huyo binadamu na baadae kidogo ikaja gari ya selikari ya walipa kodi ikasimamishwa na abiria wampeleke mgonjwa hosp kwani huko wanakokwenda ni karibu na bosi wa ile gari ambaye ni mwanamke alikataa na kuondoa gari.basi la abiria kuona hivyo nao wakaondoka.wakabaki pale SATIFA na dereva wa toyota ndipo huyo rafiki yangu akabidi kumbeba kwenye gari yake kumpeleka polisi kisha hosp usevya.sasa Mzee Mulilo polisi mlimuokoaje satfa.na isitoshe ile mbuga ya katavi mbona ina makamera kibao ukipata jam mle wanaona kila kitu.na yule dereva anasema wakati anaendesha gari walinzi wa mke katavi walikuwa wanamfuatilia na kumsimamisha na kukagua na kuwaambia amebeba mgonjwa aliyemuokota humo polini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…