TANZIA Kamanda wa Polisi Mstaafu na MwanaCCM mkongwe Zelothe Stephen afariki dunia

TANZIA Kamanda wa Polisi Mstaafu na MwanaCCM mkongwe Zelothe Stephen afariki dunia

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1698341899587.png

Kwa mujibu wa taarifa ilitolewa na Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa, kada huyo wa Chama Tawala amefariki wakati akiwa Hospitali akiendelea na Matibabu.

Nafasi ambazo amewahi kutumikia ni pamoja Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamanda wa Polisi mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma.

Pia, amewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha
 
M/kiti wa CCM Mkoa wa Arusha mzee Zelothe Stephen ameaga Dunia.

Mwendazake huyo alikuwa mtu muhimu mno kwa mikakati ya CCM hasa eneo la ulinzi na usalama!

Kabla ya awe M/kiti wa CCM Arusha mzee Zelothe alipata kuwa Afisa mwandamizi wa Polisi Tanzania.
 
View attachment 2793949
Kwa mujibu wa taarifa ilitolewa na Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa, kada huyo wa Chama Tawala amefariki wakati akiwa Hospitali akiendelea na Matibabu
Nafasi ambazo amewahi kutumikia ni pamoja Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamanda wa Polisi mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma. Pia, amewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha
Nikajua huwa hawafi? Wakiwa madarakani hujufanya miungu wadogo!
Any way R. I. P kamana na kadacwa chama
 
TANZIA: Kada wa CCM na Afisa Mwandamizi wa juu zamani wa Jeshi la Polisi Zelothe Stephen amefariki dunia leo Oktoba 26, 2023 Jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Jerry Slaa amethibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika

“Kwa masikitiko makubwa, kwa niaba ya familia, naomba uleta taarifa za kifo cha Mzee Zelothe Steven kilichotokea leo Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.”

“Mipango ya maazishi inafanywa nyumbani kwake Seaview Upanga.
Maziko yatafanyika nyumbani kwake Olasiti Arusha kwa tarehe itayotangazwa.”

“Kwa kuwa ni ngumu kumtaafiru kila mmoja , naomba mpokee taarifa hii kwa wote. Tumwombee marehemu na tuiombee familia katika kipindi hiki cha msiba.” ameandika Jerry Slaa.
 
1698342732289.jpg

Back
Top Bottom