Kamari za kwenye minada waliowahi kuliwa hela, simu nk

BALENSIAGA

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2019
Posts
3,353
Reaction score
5,800
Habari wana Chitchat

Leo nimekumbuka wale wanaochezesha kamari minadani wale jamaa wanatapeli sana watu simu,hela na pia ukiingia unawaona wako watu wengi wanacheza kumbe wote ni kitu kimoja, unaangalia unaona watu wanakula hela cheza sasa wewe uone lazima uliwe, mliowahi kutapeliwa, kuwatapeli watu karibuni tupeane uzoefu.

Nawasilisha
 
Mi na wahuni wangu wa manzese ndo ilikua michezo yetu enzi za utoto hasa karata tatu

Baadae polisi wakazingua tukaingia mjini tukawa tunauzia maboksi watu badala ya simu mwenzetu mmoja alishikwa akadundwa nusura auwawe

Tukabadili tukawa tunatapeli watu pale soko la karume plus kweny minada ya nguo tunakuuzia matambala badala ya nguo kipande cha kitenge low quality ukikifua kimevuja tunakifunga vizur tunakuuzia au tunakwambia unapata na begi bure au buku lakin lazima ununue kitu palepale tunakuwa na watu wetu wananunua kukuvutia na ukinunua hupati begi ng'oo

Tukaja na ile staili mfano umeleta beki tatu toka bushi (mikoani) sisi tunakulia radar na masela wangu siku umeenda kazini tunaenda pale tunamwambia ni mafundi umetutuma tuchukue kitu kwa ajili ya ufundi mfano friji au tunaamisha vyombo kusingizia unahama nadhani hii mliisikia kitambo sana

Na utoto wangu huo huo miaka fulani hivi karibia na ujana tukawa tunatoboa madirisha ya watu kule mafiga Moro tunavuta simu dirishani ,tushakaba watu sana chamwino enzi hizo nimekimbia dar nimeenda Moro kuepuka soo la wizi

Ila imebaki historia nshaachana nayo hayo nshakuwa mtu mzma elimu ilinikomboa na huo udhwalimu nikaamua nipige kitabu

wahuni wangu wengi wapo gereza la huko tunduma na hapo mkuranga wanamalizia malizia ada yao nadhan nao wamebadilika

Yaani ktk kipind changu cha haya matukio nimejifunza wajinga wapo kila siku na ndo hao tunaowaliza .
 
-interesting kuna Dada mmoja enzi hizo alitapeliwa hela za matumizi ya mwezi ilikuwa ni hatari kwa sababu ilikuwa vigumu sana kuamini.
 
*****...yaani hyo ya minada ya nguo usku sitosahau,japo yale manguo yanapoor quality lakini nazitimba hvyohvyo kufidia pesa yangu
 
Uthisubutu kununua nguo kwenye minada

Halafu usipende kununua nguo usiku
Napenda sana minada ya nguo za mtumba,chimbo langu kubwa ni pale buguruni bakhresa....Ila lile tukio la kununua usiku,sijui ujasiri niliutolea wapi..
 
Napenda sana minada ya nguo za mtumba,chimbo langu kubwa ni pale buguruni bakhresa....Ila lile tukio la kununua usiku,sijui ujasiri niliutolea wapi..
Hata hivyo tunajifunza kutokana na makosa mkuu


Mitumba ni mizuri lakini sio ya kwenye minada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…