Kamatakamata huko kijijini

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
Habari wana JF.

Nimepokea ujumbe kutoka kijijini kuwa rafikiyangu kipenzi amekamatwa na kuswekwa rumande kwa kosa la kushindwa kulipa kiasicha TZS 570,000/=

Issue ilikuwa hivi. Kuna jamaa huwa wananunuamazao kipindi cha mavuno hivo hutumia wenyeji wa eneo husika kama maajenti iliwaweze kupata mzigo kiurahisi.

Ilitokea akaja mtu mmoja tumiute XX,akamkabidhi rafiki yangu kiasi cha TZS 900,000 ili akusanye mzigo. Akakusanya mzigowa TZS 330,000 Kisha akamkabidhi.

Kumbe huyo XX nae alipewa hela na YY. Siku moja XX na YY wakakorofishana, hivo YY akamuombaXX amkabidhi pesa zake zote na akamkabidhi pamoja na deni la rafiki yangu. Kwa hiyo deni likabaki kati ya YY na rafiki yangu.

Baada ya siku kadhaa XX akaja akachukua mzigokwa rafiki yangu wa TZS 420,000 ambao ulikuwa tayari kwa madai ametumwa na YY. Kwavile rafiki yangu alianza kumfaham XX kabla ya YY hakupata tabu kumkabidhi ulemzigo.

Kiasi kilicho baki rafiki yangu alinunua mzigolakini hakuuchukua kwa wauzaji.
Mwenye nao anautaka tangu mwezi wa tisa. XX ametokomea hata wale alionunua nakutokuchukua mzigo nao wametokomea.
Rafiki yangu yuko kijijini alishawishiwaakubali na waandikishiane kulipa hilo deni na kisha watasaidiana kusaka haowalio kimbia wamurudishie pesa zake. Yotehayo yalifanyika.

Sasa je. Kunanjia atajinasua na Kesi hiyo.

Karibunui kwa michamgo yenu tumnusuru rafikiyangu.
 
Hizo xx an yy zinavuruga! By the way ndg Zako wa Chuo wamepata mkopo wote??
 
Katikati ya stori umechanganya ila kwanini wanafanya biashara bila mawasiliano ? Anyway muhimu ni kumchukulia dhamana rafiki ako kisha fanyeni msako wa kuwatafuta waliopotea na mizigo.
 
kwa hapo mkataba ulikuwa wa rafik yako na xx na yy hakuwepo so yy ni third part ktk hayo makubaliano na kam tunavyojuwa third part han haki ya kushtak wala kushtakiwa so yy yey alitakiwa amshtaki xx na na sio yy na ndio maan huyo ndugu yako aliamua kumalizan na xx coz ndio walio kuwa ktk biashara
 
We ulishakabidhiwa mwenye pesa yake kuwa utamlipa/kumpa mzigo, anakuja huyo aliyekukabidhi tena unampa pesa bila mawasiliano, kama wameamua kukuzunguka si watakuumiza! Umakini kwenye pesa ni jambo la msingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…