Kamati Kuu ya CCM kukutana Dodoma kesho Jumanne Juni 22, 2021

Kamati Kuu ya CCM kukutana Dodoma kesho Jumanne Juni 22, 2021

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM inatarajia kukutana kesho Jumanne Juni 22, 2021 chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Jakaya Convention Centre Jijini Dodoma.

Kikao hicho kimetanguliwa na kikao cha Secretariet ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo kimefanyika katika ukumbi wa NEC White House Jijini Dodoma

"Ni kweli Jumanne 22 Juni 2021 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ataongoza kikao cha kawaida cha kamati Kuu, maandalizi yote yamekamilika, ni kikao cha kawaida cha Kikatiba" Shaka Hamdu Shaka Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.

ChamaImara
KaziIendelee


IMG-20210621-WA0098.jpg
 
Na kesho top Leaders watakua wametoka au wamekuzwa na Upinzani, nyie mtaendelea kuimba mapambio ya kinafiki
 
Yaani kikifanyika Ikulu unaanza oh sijui nini, kisipofanyika unajifanya kuhoji kwa nini. Alimradi uonekane ni mpinzani tu kila siku. Duh.
..mimi ni mwana-ccm nimeunga mkono legacy. vikao vya kamati kuu vifanyike ikulu. kama una tatizo na hilo kunywa sumu ufe.
 
Kuna Mtu leo alikuwa anauliza mama kafuata nini dodoma, hao wateule wawili siangewaapisha Dar tu!!!,
Uyu jamaa GENTAMYCINE
Ni much know sana ,

inabidi apate taarifa kesho mama ana kikao Cha kamati kuu, ndiomaana kaenda dodoma
 
Hivi kwanini hivi vikao havifanyiki ofisi ndogo ya CCM Kisiwandui
 
Back
Top Bottom