Bado wako ndani. Alianza kuhojiwa Dk. Bilal, ambaye amehojiwa maswali makali makali ikiwa ni pamoja na kuulizwa kwanini hataki maridhiano na kwanini anaendeleza makundi na uhasama. Wakafuata wengine na Shein akawa wa pili kutoka mwisho kabla ya kumalizia Haroun Suleiman (Waziri wa ELimu).... Kwa hali ilivyo mambo ni magumu sana kwa Bilal maana tofauti na miaka ya nyuma hana nguvu CCM Zanzibar (Viongozi, ambao kwa hatua hii ndio wenye kura). Anategemea kidogo bara ambako nako kuna utata kama atapita Kamati Kuu, maana mpasuko wa CCM ndipo unapoanzia hapa. Kundi la Karume kwa sasa linamtaka Shein kwa nguvu zote na JK anatajwa kuwa nyuma yao kwa msingi wa maridhiano na mshikamano ambao unaanzia ndani ya CCM, Zanzibar na bara na kuendelea hadi CCM na CUF Zanzibar. Kwa hali ilivyo Shein anaonekana kuwa chaguo la katikati baada ya Bilal kucheza karata yake vibaya dakika za mwisho kwa kuonyesha kwamba anapinga maridhiano kati ya CCM na CUF na kuendeleza siasa za "Mapinduzi Daima" kwa kufanya hivyo anawapa nguvu watu kama Mohamed Aboud ambaye tunamuona hapa anakwazwa na kutokuwa mwaminifu katika kuwasilisha nyaraka zake za elimu. Dk. Shein kutokana na kuwa mtu wa kati kati na ambaye waatu wa bara wanaona anawazibia, ataungwa mkono apite Zanzibar na kuwa mgombea wa CCM. Kazi itakuwa katika kumuuza kwenye kampeni dhidi ya Seif wa CUF.
Kuna tatizo kubwa la kampeni. Wenyewe CCM wanasema wanao uwezo wa kumuuza mgombea watakayempitisha.
Wana JF tatizo la Zanzibar ambalo limekuwa halisemwi si la CCM na CUF ni la waliopinduliwa na waliopindua. Kuna tatizo la watu weupe na watu weusi, ni tatizo la ubaguzi ambalo waliopindua wamerithi ubaguzi kwa kuanza wao kuwabagua Waarabu kiana. Ukizungumza na watu wanaomuunga mkono Mohamed Aboud wanasema ni mtu anayefaa maana ana asili ya Kiarabu na kwamba atafanya kama Obama kuonyesha kwamba hakuna tabaka la watawala na watawaliwa. Wanasema kwa sasa Seif huwa anashinda chaguzi zote kwa sababu asilimia kubwa ya watu wa Unguja na Pemba wamechanganya wakiwamo hao watawala wanaowabagua waliochanganya. Mfano Karume mama yake ana asili ya Kiarabu, Mke wake Shadya naye ana asili ya Arabu, na kadhalika. Kwa hiyo CUF wanahitaji kuwekewa mtu atakayevunja huo ukimya si Shein vinginevyo ni kumuachia Seif aendelee kushinda na aibiwe na kuendeza vidonda visivyokwisha. Hoja hiyo ndio inayompa nguvu Haroun ambaye jina lake linaweza kupita kumsindikiza Shein hadi mwisho kama alivyowekwa Salim Ahmed na MWandosya kumsindikiza JK 2005
Tusubiri tuone. Mchakato ndio kwanza unaendelea na vita ssa ni kati ya Bilal na Shein japo wapo SHamhuna, SHamsi na Haroun.