Kamati ndogo suala la posho yaundwa! Mbowe ndani!

Tangopori

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Posts
1,628
Reaction score
1,285
Mwenyekiti wa muda wa ‪Bunge La Katiba ‬ameunda kamati ndogo ya wajumbe 6 kuchunguza suala la malalamiko ya posho juu ya bunge hilo la katiba.
Wajumbe wanaounda kamati ya kuchunguza posho ni Lukuvi, Freeman Mbowe, Paul Kimiti, Mohamed Aboud, Asha Makame na Jenista mhagama.
 
mbona wanapoteza muda maana hizo posho sio kama ni tatizo sisi tunachotaka waanze kufanya kazi ya kututengenezea katiba mpya.
 
Tangu mwanzo nilisema hatutaweza kupata katiba iliyo bora kwa kuwa mchakato mzima wa katiba mpya umetekwa na CCM ambao awali walisema hawahitaji katiba mpya kwa kuwa iliyopo inatosha.hawa jamaa wamepanga kuifisidi nchi hii hadi tone la mwisho!
 
Ndicho kilicho wapeleka Dodoma. Kwani katika hali ya kawaida wanunge hulipwa kiasi gani wanapokutana kwa vikao vya kawaida hadi leo walalamike??
 
Kwa hao waliounda hiyo kamati lazima waje na majibu ya posho iongezwe tu,wangemuweka na ZZK labda ningekuwa na imani

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Na ndio maana tangu mwanzo ilipendekezwa wajumbe wa Bunge la Katiba wateuliwe na taasisi zao bila kuhitaji uteuzi wa pili wa Rais kama ilivyofanyika. Utaratibu huu ungesaidia kuondoa upuuzi huu usio na maana wa posho na madai mengine ya kijinga kwani kila mjumbe angekwenda kuwakilisha waliomtuma pale badala ya kutumwa na Rais.

Pia lile wazo la awali lililokataliwa kwa nguvu zote na wabunge wa CCM kwamba wabunge wa Bunge la Makinda wasiwe sehemu ya Bunge Maalumu la Katiba ilikuwa na mantiki sana sema ndiooooooooo zisizo na maana ndio zimetufukisha hapa.
 
na hao wajumbe wa hyo kamati watalipwa sh ngap kwa siku???au wanajitolea tu kufanya uchunguzi kwa uzalendo?
 
Kwanini wasitoe memo, yule ambae hataki na hawezi kuishi kwa laki 3 kwa siku, ajitoe?
Mbona walimu na madoctor waliambiwa ivo?
 
Kamati tena...kweli posho ni janga la taifa..sasa kamati ya nini...wafanye kazi huko!
 
Hata hili posho linahitaji KAMATI!Ama kwa hakika Watanzania tumerogwa.....
 
Kamati ndogo ya walimu pia iundwe kuchunguza malalamiko ya walimu juu ya mishahara midogo na kuminywa marupurupu yao...
Pia kamati ndogo ya askari iundwe kuchunguza malalamiko ya askari kuhusu mishahara midogo

Ahaha nimependa majibu yako. Tayari umemaliza majibu yote

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
posho posho hiyo tume iliyoundwa inatumia pesa za walipa kodi ya nin tume. kila ck tume zinaundwa lakini haziji na majibu ya kutosha. hatuhitaji tume bali tunahitaji katiba yenye kuwafaa watanzania wote. hizi zote ni ni mbinu za kupitisha serkal 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…