Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Nauliza viongozi wote wa dini pamoja na ile inayojiita kamati ya amani iliyojitokeza kupiga marufuku matumizi ya neno mwendazake wako wapi muda huu ambapo polisi wameanza kuvamia makanisa na kukamata watu kwa kisingizio kuwa wamevaa nguo za CHADEMA.
Toka lini ikawa ni utaratibu kwa polisi kupangia waumini nguo za kuvaa wanapoenda ibadani? Mbona tumeona askari wa aina zote wakiingia makanisani na wengine kufunga ndoa wakiwa wamevaa sare za jeshi na hawajawahi kukamatwa au kutolewa kanisani?
Ni ukweli ulio wazi kuwa amani ya nchi huharibiwa na watawala kwa kutumia vyombo vyao vya mabavu kama polisi. Hakuna mahali popote wapinzani au waumini walianzisha vurugu mpaka pale polisi walipofika na kuanza kuvurumisha mabomu yao, kupiga na kukamata watu.